Trending News

CCM Adverts and Promo

Wednesday, March 23, 2016

MHE.RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AWAKUMBUKA WAZEE SHINYANGA.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Abdul Rashid Dachi akikabidhi chakula kwa Wazee wa kituo cha Kolandoto Mkoani Shinyanga kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli ametoa chakula kwa Wazee wanaoishi katika kituo cha Wazee cha Kolandoto
kilichopo Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka.

Akikabidhi chakula hicho kwa niaba ya Mhe. Rais, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Abdul Rashid Dachi, amewaeleza wazee hao kuwa Mhe. Rais anawatakia kila la heri katika Sikukuu ya Pasaka na ameahidi atakapopata nafasi atawatembelea kituoni hapo.

Naye Mwenyekiti wa Wazee hao Mzee Samwel Maganga amemshukuru sana Mhe.Rais kwa kuwakumbuka na kuwajali katika sikukuu hiyo.

Na. Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Shinyanga

No comments:

Post a Comment