Trending News

CCM Adverts and Promo

Sunday, March 20, 2016

OLE SENDEKA Msemaji mpya wa CCM



Chama cha mapinduzi (CCM) kimemteua Mbunge wa Zamani wa SIMANJIRO mkoani Manyara, CHRISTOPHER OLE SENDEKA kuwa msemaji wa chama hicho.


Akitangaza hatua hiyo katika mkutano na waandishi wa habari Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam  jijini DSM Katibu mkuu wa CCM ABDULRAHMAN KINANA amesema uteuzi wa OLE SENDEKA kuwa msemaji wa chama hicho, ni hatua ya kupunguza majukumu ya kiutendaji kwa aliyekuwa msemaji wa chama hicho NAPE NNAUYE aliyeteuliwa kuwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kinana amesema hatua hiyo itatoa fursa kwa watendaji hao kutimiza majukumu yao kwa ufanisi zaidi  katika kuwatumikia wananchi.

Akizungumza mara baada ya uteuzi huo,msemaji huyo wa CCM CHRISTOPHER OLE SENDEKA ametoa wito kwa wanasiasa nchini kuacha siasa za  kuponda jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kutimiza majukumu yake, ambapo amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi.

No comments:

Post a Comment