JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
|
OFISI YA RAIS,
IKULU, 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi, kufuatia kifo cha ghafla cha Mkuu
wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, Kilichotokea jana jioni tarehe 21 Machi,
2016.
Bi. Sara Dumba
aliugua ghafla kuanzia jana mchana na baadaye kukimbizwa katika hospitali ya
Mkoa wa Njombe (Kibena), ambako wakati akipatiwa matibabu alifariki dunia
majira ya saa moja za jioni.
Katika salamu hizo
Rais Magufuli ameelezea kushitushwa na kifo cha ghafla cha Bi. Sara Dumba,
ambaye amesema alimfahamu kwa uchapakazi wake, uaminifu na uadilifu katika
utumishi wa umma na katika uongozi.
"Nimeshitushwa
sana na kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, kwa mara nyingine
Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye mchango wake ulikuwa bado unahitajika"
amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli
amebainisha kuwa Marehemu Sara dumba atakumbukwa kwa kazi kubwa aliyoifanya ya
kuhimiza maendeleo ya wananchi, hususani katika kilimo na ufugaji, kuhimiza
nidhamu ya utumishi serikalini na kuwatetea wananchi wa hali ya chini wakati
wote wa majukumu yake ya ukuu wa wilaya.
Rais Magufuli
amesema anaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote
walioguswa na msiba huu mkubwa, katika kipindi hiki kigumu na pia amewataka
wote kuwa na subira na uvumilivu.
Amemuombea kwa
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam.

No comments:
Post a Comment