Trending News

CCM Adverts and Promo

Monday, March 21, 2016

WAZAZI MKOA WA MOROGORO WATOA MSAADA WA MAHINDI KWA WANANCHI WALIOATHIRIWA NA MAFURIKO MOROGORO

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ndugu Fadhili Liguguda akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Morogoro Bi. Mecktridis Mdaku.
Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Morogoro Bi. Mecktridis Mdaku ametoa msaada wa mahindi kwa wananchi walioathiriwa na mafuriko katika maeneo ya Malinyi, Usangule na Itete.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Bi. Mdaku, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ndugu Fadhili Liguguda amesema kuwa, Msaada huo uliogharimu shilingi milioni moja(1,000,000/=) umekabidhiwa kwa wananchi wa maeneo husika.


Ndugu Liguguda, amewaomba wananchi hao kutumia msaada huo kwa malengo yaliyokusudiwa. Aidha, wananchi hao kuendelea na kilimo kwani bila kilimo watakumbwa na baa la njaa.

Amemshukuru Bi. Mdaku kwa msaada alioutoa na aendeelee kuwa na moyo kama huo wa upendo na unyenyekevu  kwa wananchi wowote wanaokumbwa na majanga kama hayo.



Kwa upande wao wananchi wa Itete, Usangule na Malinyi wamemshukuru mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Morogoro bibi. Mecktridis F.Mdaku kwa msaada aliowapatia. Wamemuomba azidi kushirikiana nao katika majukumu ya kujenga Taifa letu.

No comments:

Post a Comment