
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Jerry Sabi (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya CreditInfo Tanzania Ltd Bw. Davith Kahwa wakisaini mkataba ambao utaiziwezesha taasisi za kifedha zinazotoa mikopo nchini kuhakiki taarifa za waombaji mikopo, ambao ni wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, kabla ya kuwapa mikopo mipya. Wengine ni Bw. Frimat Tarimo, Mwanasheria wa HESLB na Bw. Van Reynders, Meneja wa CreditInfo Tanzania.
Na Mwandishi Wetu - Dar es salaam.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) mwishoni mwa wiki imesaini mkataba na Kampuni ya CreditInfo Tanzania Ltd utakaowezesha taarifa za wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kufikishwa katika Kitengo Uratibu za Taarifa za Mikopo (Credit Reference Bureau) kilichopo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kampuni ya CreditInfo Ltd ina leseni iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
Hivyo basi, mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambaye ataomba mkopo kutoka kwenye taasisi yoyote ya kifedha hapa nchini, taasisi hiyo itakuwa na uwezo wa kuhakiki kama mwombaji huyo ni munufaika wa mkopo wa elimu ya juu na ikiwa ana nidhamu ya kurejesha mikopo.
No comments:
Post a Comment