Mtaalam wa Jiografia
kutoka Chuo Kikuu Ardhi Dkt. Mlenge Fanuel Mgendi akiwahamasisha wanafunzi wa kidato cha Sita
wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani
kupenda kusoma na kuweka bidii katika masomo ambayo wana uwezo nayo ili
yawasaidie kuendelea na Elimu ya Juu katika chuo Kikuu Ardhi na vyuo vingine leo jijini Dar es
salaam. Chuo Kikuu Ardhi kinaendesha Programu ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa
sekondari katika shule mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia kufanya uchaguzi sahihi wa kozi za masomo
wanazotarajia kuendelea nazo pindi watakapohitimu masomo ya elimu ya Sekondari.
Mwanataaluma wa Chuo Kikuu Ardhi Bi. Latifa
Litwe (kushoto) akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana
ya Jangwani namna ambavyo Chuo Kikuu Ardhi kinawajengea uwezo kielimu wanafunzi
wanaosoma katika chuo hicho kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi na majanga
mbalimbali yanayoihusu sekta ya Ardhi kwa ujumla pamoja na masuala ya uhifadhi
wa Ardhi na Sayansi ya Udongo.
Baadhi ya wanafunzi
wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani wakiangalia na
kufurahishwa na moja ya Kazi ya Ubunifu wa Majengo na mitaa iliyofanywa na wanafunzi
wa Chuo Kikuu Ardhi mwaka wan nne leo jijini Dar es salaam.
Mwanataaluma wa
Chuo Kikuu Ardhi Bw. Dennis Tesha akiwaeleke za wanafunzi wa shule ya wasichana
ya Jangwani namna bora kuchagua masomo yao ya baadaye kulingana na sifa
walizonazo watakapotaka kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini pamoja na kazi
watakazofanya mara baada ya kuhitimu kulingana na masomo yao.
Moja ya kazi ya Ubunifu
wa jengo refu la ghorofa lilobuniwa na mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi.
Baadhi ya wanafunzi
wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani wakifurahia jambo mara
baada ya kuangalia moja ya kazi ya ubunifu wa majengo iliyofanywa na wanafunzi
wa mwaka wan ne wa Chuo Kikuu Ardhi walipokuwa wakizungumza na Afisa Uhusiano
Mwandamizi wa Chuo hicho Hadija Maulid leo jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Zanaki ya jijini Dar es salaam wakimsikiliza kwa makini Mhadhiri
Msaidizi-Uhasibu na Usimamizi wa Fedha wa Chuo Kikuu Ardhi wakati wa programu
maalum ya Chuo hicho ya kuwaelimisha wanafunzi wa shule za Sekondari kuhusu masuala
mbalimbali ya kitaaluma kuhusu sekta ya Ardhi yanayofundishwa na chuo hicho leo
jijini Dar es salaam.
![]() |
| Baadhi ya machapisho ya Chuo Kikuu Ardhi wakati wa Programu hiyo. |
Mbunifu Majengo
kutoka Chuo Kikuu Ardhi Bw. Jafer Salehe Jongo akiwafafanulia baadhi ya
wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani Kazi ya Ubunifu
wa Majengo na mitaa iliyofanywa na wanafunzi wa Chuo hicho walioko mwaka wa nne
leo jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakiangalia Machapisho kuhusu masuala
mbalimbali yakiwemo ya upimaji wa Ardhi, Uthaminishaji wa majengo, Mazingira,
Mipango miji yaliyotolewa na Chuo Kikuu Ardhi leo jijini Dar es salaam wakati
wa program maalum ya kuwapatia elimu waanafunzi wa shule za jiji la Dar es
salaam kuhusu Chuo Kikuu Ardhi.











No comments:
Post a Comment