Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
amefanya uzinduzi wa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa Kanda ya
Mbeya.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema uzinduzi
wa duka hilo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais
Magufuli kuwatia wananchi huduma bora na kwa gharama
nafuu. “Neema
hii imekuja kwa kipindi cha Rais Magufuli, sasa amekidhi matakwa na shauku
ya wananchi wa Mbeya kwa kuwapa duka la dawa"
Ameeleza kuwa Sera
ya huduma ya afya inataka wananchi wachangie isipokuwa wazee, watoto na
wajawazito na kupitia duka hilo wananchi wataweza kupata dawa kwa gharama
nafuu,” amesema Mhe. Mwalimu. Duka
hilo la dawa la Kanda ya Mbeya limetumia Shilingi Milioni 13 kwa ukarabati
wa jingo na vifaa vyake.
Mh.Ummy Mwalimu akionesha moja ya dawa inayouzwa
dukani hapo kwa shilingi 7,000 ambapo kwenye maduka binafsi inauzwa
shilingi 25,000,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurine Bwanakunu na
kulia ni Mfamasia wa duka hilo, Cornel Mkeng'e
Mfamasia wa Duka la Dawa, Cornel Mkeng'e akitoa
maelezo kwa Mh.Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua duka
hilo.
No comments:
Post a Comment