Trending News

CCM Adverts and Promo

Sunday, April 17, 2016

HATUTAMWONEA MTU UTUMBUAJI WA MAJIPU.



Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

****************************************************************************
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema serikali haina nia ya kumwonea mtu, inapochukua hatua ya kutumbua majipu kwa watumishi wa umma.

Amesema lengo la kutumbua majipu ni kurekebisha na kurejesha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji serikalini, kama ilivyoangizwa katika Ilani ya Chamaq Cha Mapinduzi (CCM) ili Watanzania wote wafaidike na matunda ya nchi yao.

“Mtasikia katika serikali majipu yanatumbuliwa hatuna nia ya kumwonea mtu, tunarekebisha kama ilivyoagizwa katika Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi ili Watanzania wote wafaidi matunda ya nchi yao,” amesema Samia.

Amesema katika marekebisho hayo, serikali imechukua hatua ya kukata mishahara ya walio juu na kunyanyua ya walio chini waje juu kidogo na kwamba jitihada zote hizo ni katika kufanya mambo yaende vizuri nchini.

No comments:

Post a Comment