Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi
ndugu Fadhili Liguguda akizindua boti itakayofanya kazi ya usafirishaji wa abiria katika
mto Mnyera uliopo Malinyi mkoani Morogoro.
Baadhi ya wananchi wakishuhuhudia boti hiyo ikiingizwa
mto Mnyera uliopo Malinyi mkoani Morogoro.
Boti hiyo ikianza kazi ya kuvusha watu ndani ya mto Mnyera
Na. Mwandishi Wetu - Morogoro.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi
ndugu Fadhili Liguguda amezindua boti itakayofanya kazi ya usafirishaji katika
mto Mnyera uliopo Malinyi mkoani Morogoro.
Akizindua
chombo hicho cha usafirishaji amesema kuwa Boti hiyo itarahisisha utendaji wa kazi
husususan wananchi kuwezeshwa kuvuka kutoka eneo moja la mto hadi lingine kwa
urahisi zaidi tofauti na awali ambapo walikuwa wakipata shida wakati kipindi cha
mvua.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Malinyi ndugu Said Msolmoka
akizungumza wakati wa makabidhiano kivuko hicho amesema kuwa kimegharimu fedha
za kitanzania shilingi milioni tisa(9,000,000/=).
Ndugu
Msomoka amewaomba wananchi na wahusika wanaoisimamia boti hiyo kuitumia kwa
uangalifu na kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kwa
upande wao wananchi wa Malinyi wameishukuru halmashauri hiyo kwa msaada huo ilioutoa
wakieleza kuwa hapo awali maisha yao yalikuwa hatarini kwa kuliwa na mamba
kutokana na kukosekana kwa usafiri wa uhakika.
Wananchi
hao wamemuahidi mkurugenzi huyo kuwa watakitunza chombo hicho na kukitumia kwa
kazi iliyokusudiwa.
Katika
hatua nyingine uongozi wa wilaya ya Malinyi umetembelea Hospitali ya Lugalo iliyomo
Malinyi na kupanda miti 1500 na kufanya
usafi wa mazingira.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya usafi wa mazingira na kupanda
miti Mkurugenzi wa wilaya hiyo ndugu Said Msolomoka, amesema Wilaya yake
inamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika suala la
usafi.
Amesema
kama Halmashauri ya wilaya wametenga siku maalum kila mwanzo wa mwezi kwa ajili usafi.




No comments:
Post a Comment