Trending News

CCM Adverts and Promo

Saturday, April 16, 2016

WILAYA YA KAHAMA YAPEWA SIKU 90 IWE IMENUNUA MASHINE YA X- RAY


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiongea na baadhi ya wakazi wa kahama waliofika hospitalini hapo kuangalia wagonjwa wao.


Na.Catherine Sungura - Kahama.

Mkurugenzi wa halmashauri  wa mji kahama  amepewa siku tisini awe  amenunua mashine ya mionzi (x ray)kwa ajili ya hospitali ya mji kahama.

Agizo hilo amepewa jana na Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu wakati alipotembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa kada ya afya wa wmji huo.

Waziri Ummy alisema ametoa agizo hili ili kuweza  kurahisisha usumbufu wanaupata wananchi wa wilaya hiyo kwa kwenda kupata huduma  nje ya hospitali ambapo wakati mwingine vipimo hivyo vinakuwa havisomeki vizuri kwa kukosa viwango vinavyostahili za mashine hizo.

Hata hivyo waziri ummy alisema upatikanaji wa mashine hizo itapunguza malalamiko mengi toka kwa wananchi kwa ukosefu wa kifaa tiba hicho   kwani hospitali hiyo hivi sasa inahudumia wananchi zaidi ya milioni moja hususan toka wilaya zote za wilaya hiyo.

Aidha, alizitaka halmashauri zote mjini kuweza   kuwekeza kwenye huduma za vifaa tiba  ambavyo inarahisisha kugundua  matatizo yanayowakabili wananchi wanaofika kwenye kupata huduma na hivyo kuwapatia matibabu stahili wagonjwa wanaofika kupata matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.

“siku hizi lazima muwekeze  kwenye kununua vifaa tiba ili kuweza kupata kutoa huduma nzuri ,pesa mnakusanya na kahama ni halmashauri tajiri,mkurugenzi  nakupa siku tisini uwe umenunua mashine hiyo

Naye mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Vita kawawa amemuahidi waziri huyo kwamba amepokea maagizo yote aliyoyatoa na atayafuatilia ili kuweza kutatua malalamiko ya wananchi na yale ya watumishi wa kada ya afya.

No comments:

Post a Comment