Trending News

CCM Adverts and Promo

Thursday, May 5, 2016

MSANII SNURA MUSHI ATUBU MBELE YA WATANZANIA KUTOKANA NA WIMBO WAKE WA CHURA AAHIDI KUFUATA MAADILI KATIKA KAZI ZAKE.


Msanii wa kizazi kipya Snura Mushi (kulia) akiomba msamaha mbele ya Watanzania kutokana na kusambaza video yake iliyokiuka maadili ya Kitanzania maarufu kama ''Chura'' mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msimamizi wa kazi zake Bwana Hemed Kavu maarufu kama HK.
Msimamizi wa kazi za Snura Mushi Bwana Hemed Kavu maarufu kama HK (kushoto) pamoja Msanii wa kizazi kipya Snura Mushi wakionyesha Cheti alichokabidhiwa Bi Sunra Mushi na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa ajili ya kuruhusiwa kufanya kazi zake za kisanaa nchini.

                           ****************************************************************************

Msanii Wa Bongo Fleva Snura Mushi (Snura) amewaangukia Watanzania kwa kuwaomba  radhi watanzania  kwa usumbufu aliousababisha wa kutoa video ya Wimbo ujulikanao kwa jina la Chura usiofuata maadili ya Kitanzania.Pia ameviomba radhi vyombo vya serikali vinavyosimamia sekta ya sanaa kwa kutokufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa sanaa.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, radhi hiyo imekuja mara baada ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo jana kufungia video ya wimbo wa msanii huyo wa Chura ikiwa ni pamoja na kutoonyeshwa kwenye Televisheni pamoja na kupigwa kwenye redio. Amesema kuwa tayari  video ya wimbo huo ameshatoa kwenye mtandao wa kijamii wa Youtube.

No comments:

Post a Comment