Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Benno Sanga akifafanua kuhusu matumizi ya sheria ya
manunuzi ya umma na umuhimu wake leo Jijini Dodoma.
 |
Baadhi ya Mawakili wa Serikali waliohudhuria semina hiyo wakisikiliza kwa makini mafunzo hayo yaliyofanyika leo Mjini Dodoma.
|
Na. Jacquiline Mrisho, Dodoma
Serikali
imezitaka taasisi zake zote kufuata sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na
taratibu zake kwa manunuzi mbalimbali ya vifaa vya ofisi ili kuhakikisha fedha
iliyotumiwa inalingana na huduma iliyopatikana.
Hayo
yamesemwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benno Sanga kwenye Mafunzo ya Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 kwa Mawakili wote
nchini iliyofanyika mjini Dodoma.
Mafunzo
hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, yamelenga kuwapa
mawakili ujuzi katika utoaji mzuri wa ushauri wa kisheria kwa Taasisi za
Serikali.
Wakili
Mwandamizi Sanga alisema kuwa msingi mkubwa wa sheria hiyo ni ushindanishwaji
wa wazabuni unaoweza kuiletea Serikali thamani ya fedha.
“Kila
taasisi ya serikali lazima ifuate sheria ya manunuzi kwa manunuzi mbalimbali ya
vifaa vya ofisi,sheria hii imeweka utaratibu wa kuhakikisha fedha iliyotumiwa
inalingana na huduma inayopatikana”,alisema
Sanga.
Akitoa
mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Mikataba (Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali) Bi.Monica Otaru alisema mafunzo hayo yatawasaidia mawakili kufanya
upekuzi wa mikataba kwa makini na uhakika zaidi.
“Pamoja
na kuwa kazi ya kupekua mikataba ni sehemu ndogo ya kazi zetu lakini inachukua
muda mwingi, hivyo mafunzo haya yatawaandaa Mawakili wa Serikali walioko katika
Ofisi za Kanda kuweza kufanya upekuzi wa mikataba kwa umakini na uhakika
zaidi”,alisema Bi. Otaru.
Aidha,
Bi. Otaru amezitaja baadhi ya changamoto zinazosababisha kazi ya uhakiki wa mikataba
kutofanyika kwa usahihi zikiwemo za mikataba kukosa maelezo na maoni kamili ya
taasisi husika.
Alitaja
changamoto nyingine kuwa ni gharama za kusafirisha mikataba kutoka taasisi
husika,ugumu wa njia za mawasiliano pamoja na kutoshirikishwa kwa taasisi
husika katika mchakato wa manunuzi na uandaaji wa mikataba.
Naye
Wakili wa Serikali Mwandamizi Divisheni ya Mikataba, Said Kalunde ameelezea juu
ya mambo muhimu ya kuzingatia katika kufanya upekuzi wa mikataba ya
ununuzi ikiwemo ujazaji wa fomu
mbalimbali zinazotumika katika uhakiki wa mikataba kwa mujibu wa Sheria hiyo ya
manunuzi.
“Ni
muhimu sana kwa wakili kujiridhisha kama taratibu za ujazaji wa fomu zimefuatwa
na fomu zimejazwa kwa usahihi,endapo wakili hatojiridhisha kwa kuhakiki fomu
hizo huenda akapatwa na matatizo makubwa ya kiutendaji”,alisema Kalunde.
Mafunzo
hayo yametolewa kwa mawakili wa serikali divisheni ya mikataba ili kuwajengea
uwezo wa kutekeleza jukumu la kuhakiki mikataba inayotokana na wazabuni.
Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeundwa chini ya kifungu cha 59 cha Katiba ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mshauri
wa masuala ya kisheria kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini
ya kifungu cha 59(3) cha Katiba ya mwaka 1977.
|
No comments:
Post a Comment