Trending News

CCM Adverts and Promo

Thursday, May 19, 2016

TASWIRA ZA WAHE: WABUNGE NJE NA NDANI YA UKUMBI WA BUNGE.

Waziri wa Nishati na Mdini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi mara walipokutana Bungeni mjini Dodoma wakati wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madinileo 19 Me, 2016  bungeni hapo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Profesa Jumanne Maghembe akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi katika Bunge hilo leo 19 Mei, 2016.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge mwenzie wakiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi katika Bunge hilo leo 19 Mei, 2016.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi katika Bunge hilo leo 19 Mei, 2016.
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa CHADEMA, Mhe. Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay wakati walipowasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya Vikao vya asubuhi vya bunge hilo leo 19 Mei, 2016.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto) akiwa na Mbunge mwenzie wakiingia ndani ya bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya asubuhi vya bunge hilo leo 19 Mei, 2016.

Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi katika Bunge hilo leo 19 Mei, 2016.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akijibu Maswali ya Wabunge.

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Andrew Chenge (kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Mhe. Cecilia Paresso wakielekea ndani ya Bunge kwa ajili ya Vikao vya asubuhi vya bunge hilo 19 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wa Majimbo mbalimbali wakiwasili katika viwanja vya bunge kuhudhiria vikao vya asubuhi ndani ya bunge hilo mjini Dodoma leo 19 Mei, 2016.

Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (mwene gauni la kitenge) akiwa na baadhi ya Wabunge wakielekea ndani ya bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya bunge hilo 19 Mei, 2016 mjini Dodoma.


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akielekea ndani ya bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya bunge hilo 19 Mei, 2016 mjini Dodoma.
(Picha/Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma)


VIWANDA VIPYA KUJENGWA ILI KUKABILIANA UPUNGUFU WA SUKARI.

Na Tiganya Vincent, Dodoma.

Serikali inaendelea na mazungumzo na wawekezaji  wanaokusudia kuwekeza katika viwanda vya  sukari ili kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati akijibu maswali ya papo kwa papo ya kila Alhamis.

Alisema kuwa lengo la mazungumzo ya kutaka viwanda viweze kuongeza uzalishaji wa sukari ili uweze kufikia tani 420,000 katika kipindi miaka minne ijayo na hivyo kupunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vipya ya Sukari ni pamoja na Kigoma, Morogoro na Bonde la Rubada lilipo katika mto Rufiji.

Kuhusu kutojengwa kiwanda cha Sukari katika eneo la Bagamoyo , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ilikataa kuruhusu ujenzi wa kiwanda cha Sukari katika eneo hilo baada ya Kamati ya Bunge kushauri kuwa kisijengwe kwa sababu kingehatarisha uhai wa wanyama waliomo katika Mbuga ya Saadan kwa kuwa kingetumia maji mengi kutoka Mto Wami.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa   hali hiyo ingesababisha upungufu wa maji ambayo ni tegemeo kwa wanyama wa Mbuga ya Saadan yambao ni muhimu kwa sekta ya utalii nchini.


UPUNGUFU WA SUKARI.


Kwa upande wa upungufu wa sukari nchini , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imeagiza  tani  70,000 kutoka nje ya nchi.

Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na kuwepo kwa upungufu wa tani 100,000.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana upungufu huo imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa Sukari nje wasije wakaingiza sukari nyingi kinyume cha inayohitajika na hivyo kuathiri viwanda vya hapa nchini.

Aliongeza kuwa Bodi  hiyo kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato nchini (TRA ) itasimamia kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza nchini ndio inayohitajika. 

Kuhusu bei elekezi ya sukari , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka kiwango ili kumlinda mwananchi wa kawaida.

Alisema kuwa bei hiyo zinazingatia gharama zote ikiwemo usafirishaji kutoka zinapoagizwa na kumfikia mlaji.

WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU LUMBESA


Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema kuwa ni kosa kwa wanunuzi wa mazao ya wakulima kununua mazao kwa vipimo visivyo halali ambavyo havikuidhinishwa na Wakala wa Vipimo nchini.

Amewaagiza viongoizi wote wa Halmashauri,Wilaya na Mikoa yote  nchini kuhakikisha wakulima hawanyonywi kupitia wananunuzi mazao kuliko vipimo halisi kama vile Lumbesa.

Mhe. Majaliwa amewaagiza Kamati za Ulinzi na Usalama katika za mikoa na wilaya kusimamia zoezi hili ili mkulima alipe kwa vipimo halali ambavyo ni kilo au gunia liloshonwa kiwanda na sio lile liloongezewa kichuguu(lumbesa).


ELIMU YAONGEZA IDADI YA WATOTO WANAOINGIA LA KWANZA


Kuhusu suala la elimu bure, Waziri Mkuu amesema kuwa lengo ilikuwa na lengo la kumpunzia mzazi mzigo wa ada ya shule za Msingi na Sekondari.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa ada hizo zilikuwa ni kati ya shilingi elfu 20 na elfu 70.
Amesema kuwa sehemu imebebwa na Serikali ni pamoja na maji,ulinzi,umeme na gharama za mitani mbalimbali.

Aidha, Mhe. Majaliwa alisema kuwa baada ya mpango huo wa elimu bure kumekuwepo na ongezeko kubwa na watoto waliondikishwa kujiunga darasa la kwanza mwaka huo  na hivyo kusababisha changamoto ya upungufu wa madawati na madarasa.
Alisema kuwa Serikali inaendelea kuzifanyia changamoto hizo na kutoa wito wadau mbalimbali kuungano mkono juhudi hizo za Serikali.




No comments:

Post a Comment