Trending News

CCM Adverts and Promo

Tuesday, June 21, 2016

JWTZ YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZILIZOTOLEWA NA GAZETI LA DIRA

 Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekanusha taarifa zilizoandikwa leo na gazeti la Dira zikidai kuwa kifaru cha jeshi hilo kimeibiwa. 

Msemaji wa Jeshi hilo Kanali Ngemela Lubinga amesema kuwa taarifa hizo si za kweli na za upotoshaji zenye lengo la kuchafua taswira ya jeshi hilo na taifa kwa ujumla. 

 Kanali Lubinga amesema kuwa Jeshi limesikitishwa sana na taarifa hizo za upotoshaji na kulitaka gazeti la Dira kuomba radhi mara moja vinginevyo hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao. 

 Amesisitiza kuwa ulinzi na usalama kwenye maeneo ya Jeshi uko imara hivyo watanzania wasiwe na hofu yoyote na wapuuze taarifa hizo za uzushi.

No comments:

Post a Comment