Jaji
Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani)wakati wa hafla ya uapisho
ya Jaji Kiongozi na Jaji wa Mahakama ya rufani leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Shaban Lila akisaini hati ya kiapo mbele
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa
hafla ya uapisho ya Jaji Kiongozi na Jaji wa Mahakama ya rufani leo Ikulu
Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
picha ya Pamoja na Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali (kulia) na Jaji wa
Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Shaban Lila baada
ya kuwapisha leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha
ya Pamoja na baadhi ya viongozi wakuu wa nchi wakati wa kutoka kulia ni Jaji Mkuu Mhe.
Chande Othuman, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, Jaji Kiongozi Mh. Ferdinand
Wambali, Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe.
Shaban Lila na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu
Mtendaji
Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Hussein Kattanga akimweleza jambo Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya
uapisho ya Jaji Kiongozi na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo Ikulu Jijini Dar es
Salaam
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Hussein Kattanga. Kutoka kulia ni
Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi.
Jaji
Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali (kulia) na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Shaban Lila wakisubiri kuapishwa leo Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
Na. Magreth Kinabo - Dar es salaam.
Jaji wa Mahakama ya Rufani
Tanzania, Mhe. Shaban Lila na Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.
Ferdinand Wambali, wamesema kwamba watafanya kazi kwa ushirikiano na
majaji wenzao ili kuhakikisha kwamba mashauri yanasikilizwa kwa
wakati, ikiwemo kuwa karibu na wananchi.
Kauli hizo zimetolewa leo
na majaji hao, mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika
hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dares Salaam.
Rais Magufuli amewaapisha
Majaji wa Mahakama hizo kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani Novemba 05,
2015.
Akizungumza
baada kuapishwa Jaji Lila alisema atafanya kazi ya kusimamia na kuongeza nguvu ili kuhakikisha mashauri
yaliyopo mahakama ya Rufani (T) yanasikilizwa na kutolewa maamuzi
kulingana na muda uliopangwa.
Kwa upande wake Jaji
Wambali, aliongeza kwamba atashirikiana na wananchi wote na pia katika utendaji
kazi wake atazingatia sheria, kanuni na taratibu, ikiwemo kutofanya upendeleo
wa husda.
“Nitafanya kazi kwa bidii,
lazima tushirikiane na wananchi wote. Nitahakikisha
Mahakama inakuwa karibu na wananchi kwa kuwafikia maeneo walipo ili kuwaondolea
kero ya kutumia muda wa siku mbili kwa ajili ya kuhudhuria kesi mahakamani hususani
kipindi cha masika. Hivyo tutatumia Mahakama za kutembea,” alisema Jaji Wambali.
Akitolea mfano wa muda wa kusikiliza kesi kwa mujibu wa kiwango cha kimataifa kesi za madai
zinatakiwa zisidi kipindi cha miaka
miwili na shauri lisizidi miezi 18.
Alifafanua kwamba kwa upande
wa mahakama za mwanzo atajitahidi kutatua changamoto zilizopo mfano kuongeza
idadi ya mahakama na fedha ili kuongeza miundombinu ya kuwafikia wananchi.
Hafla hiyo, ilihudhuriwa na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu
wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman na Watendaji wa mahakama mbalimbali,
baadhi ya majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mahakama Kuu yaTanzania,
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, na baadhi ya wageni mbalimbali.
Kabla ya uteuzi huu, Mhe.
Jaji Lila alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mhe. Wambali
alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA).






No comments:
Post a Comment