NA
ELISA SHUNDA,Dar
CHAMA
cha Wasambazaji wa Filamu Tanzania na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) vimepongeza
hatua iliyochukuliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia
waziri wake,Nape Nnauye katika kuhakikisha wanatokomeza waharamia na uuzaji wa
kazi za wasanii bila kufuata utaratibu za kisheria zilizowekwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama cha wasambazaji wa filamu
nchini,Moses Mwanyilu,alisema kuwa hatua ya serikali imekuja katika muda
muafaka kufuatia kilio cha muda mrefu kutokana na baadhi ya wafanyabiashara na
wasambaji wa filamu na muziki kutoka nje ya nchi wamekuwa wakiingiza na kuuza
bidhaa hizo bila ya kufuata utaratibu ikiwemo kulipa kodi.
Amesema
kuwa wafanyabiashara hao pia wamekuwa wakidurufu filamu za ndani ya nchi na
kuziingiza sokoni bila ya wasanii kunifaika na kazi zao ikiwemo kazi hizo
kutolipiwa kodi hivyo kupelekea kuziuza kwa bei ya chini ukilinganisha na
filamu hapa nchini jambo ambalo linasababisha soko la filamu za ndani
kudidimia.
Aidha
Mwanyilu ameongeza kuwa baada ya kilio
cha muda mrefu hatimaye wameona jitihada za serikali kupitia kwa wizara
inayohusika na masuala ya sanaa kuanza kuchukua hatua za makusudi kufanya
oparesheni ya nguvu ya kukamata walanguzi wa kazi za wasanii nchini katika maeneo
ya kariakoo.
Kwa
niaba ya chama cha wasambazaji wa filamu na shirikisho la filamu Tanzania na
vyama vyote vya shirikisho wanapenda kutoa shukrani za dhati kwa wizara ya
habari kupitia waziri wake,Nape Nnauye kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania
(TRA),Bodi ya filamu,Cosota na Baraza la Sanaa Tanzania kwa kuwa mstari wa
mbele katika kuhakikisha kazi za wasanii nchini zinauzwa kwa kufuata utaratibu
uliowekwa na unaotambulika.
Naye
Katibu Mkuu wa chama cha Wasambaji wa Filamu Tanzania,Suleiman Ling’ande
alisema kuwa tatizo la uharamia katika kazi za wasanii nchini ni changamoto ya
muda mrefu kufuatia kuwepo na sheria ambayo imeshindwa kukidhi na kusimamia
utaratibu unaofaa hasa katika kuhakikisha kazi za wasanii zinawanufaisha
wasanii pamoja na kuliongezea kipato taifa pamoja na kulipa kodi.
Pia
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifamba,amesema kuwa
anaunga mkono zoezi linaloendelea kwa wadau wa kazi za wasanii cnhini
wakishirikian na serikali katika kuhakikisha wanatokomeza uharamia wa kazi za
wasanii wote nchini ili walau kuwapa motisha ya maisha mazuri waigizaji hao ili
waendelee kutengeneza kazi nzuri za kuelimisha jamii.
No comments:
Post a Comment