Picha na: Eliphace Marwa
Habari na: Frank Shija
Serikali kuwachukulia hatua kali ikiwemo
kutaifisha mitambo yao watu wote wanaojihusisha na uhalifu wa kughushi Nyaraka
za Serikali na kuwataka wananchi
wasiowaamnifu wanaojihusisha na uhalifu wa kughushi na matumizi ya Nyaraka bandia
waache mara moja.
Onyo hilo limetolewa na Mpiga Chapa
Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassian Chibogoyo katika
Kipindi maalu cha “Tujikumbeshe” ambapo alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa
kukamatwa kwa Nyaraka mbalimbali za Serikali leo jijini Dar es Salaam.
Chibogoyo amesema mwaka 1999 Serikali ilitoa tamko kupitia
Tangazo GN Na. 488 lililolenga kutahadharisha umma kuwa yeyote atakaye
jihusisha na uchapaji wa Nyaraka bandia mitambo yake itataifishwa.
Serikali imekuwa ikiendesha Operesheni
maalumu ijulikanayo “Okoa Pato la Taifa” ambayo lengo lake kuu ni kuhakikisha
inapambana vilivyo na uharamia wa matumizi ya Nyaraka bandia.
Aliongeza kuwa uhalifu wa kutengeneza Nyaraka
bandia ni zaidi ya ujambazi kwani zinaweza kuvuruga mipango ya nchi, na
kusasabisha nchi kuingia katika hatari na machafuko.
Kwa mujibu wa Sheria za nchi matumizi
ya Nyaraka bandi ni kwenda kinyume na sheria za nchi na adhabu zake
zinafahamika. Akizitaja baadhi ya Sheria hizo Mpiga Chapa Mkuu amesema makosa
ya uhalifu wa Nyaraka yanaangukia katika Sheria za Ushahidi,Sheria ya Makosa ya
Jinai, Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 1970 pamoja na Sheria ya Nembo na
Alama za Taifa.
“Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka
1970 namba 3 ibara ya 6 inatoa katazo kwa mtu yeyote kumiliki Mihuri ya
Serikali, Nembo ya Taifa na Karatasi maalum za Serikali kwa matumizi binafsi, mtu
akikiuka sheria hii adhabu yake ni miaka 20 jela”. Alisema Chibogoyo.
Aidhi ametumia fursa hiyo kwaomba
wananchi w
ema kushirikiana na Serikali kupambana na vita hii kwa kutoa taarifa
pindi wanapobaini waharifu wa namna hiyo kwani kuruhusu hali hii iendelee ni
kuhujumu uchumi wa nchini.
Aliongeza kuwa Ofisi yake kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi wamejipanga kuhakikisha wanashinda vita hii ili
kunusuru uchumi wa Taifa nakuahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi wasamaria
wema watakao toa taarifa juu ya uhalifu huo.
Baadhi ya Nyaraka ambazo zimekuwa
zikighushiwa mara kwa mara ni pamoja na Vyeti vya Elimu katika ngazi
mbalimbali, Risiti za Serikali, Vyeti vya kuzaliwa na Ndoa, Stika za Bima, Kadi
za Magari na Pikipiki, Mihuri na Nembo ya Taifa.





No comments:
Post a Comment