Picha/Habari Na Jacquiline Mrisho
Jumla
ya vijana 559 waishio katika mazingira magumu wamehitimu elimu ya ufundi katika
Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) chini ya mradi unaosimamiwa na
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Plan International.
Takwimu
hizo zimetolewa leo na Mkurugenzi wa Shirika hilo, Jorgen Haldorsen wakati wa
mahafali ya kwanza ya vijana hao yaliyofanyika katika Chuo cha VETA, jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
huyo amesema kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni kubwa na linahitaji jitihada za
pamoja katika kulikabili hivyo, kwa Mkoa wa Dar es Salaam, mradi huo unalenga
kufikia vijana 2110 ndani ya miaka mitatu kutoka Wilaya za Ilala na Temeke.
“Mahafali
ya leo ni mahsusi kwa ajili ya vijana wanaoishi katika mazingira magumu, wamesoma
fani mbalimbali za ufundi zikiwemo za umeme wa majumbani, ushonaji, udereva,
ufundi magari, uchomaji vyuma, mapishi na mapambo ambapo zaidi ya ufundi stadi
vijana wetu wamejengewa utamaduni wa kujiwekea akiba kupitia vikundi vya hisa”,
alisema Haldorsen.
Haldorsen
amefafanua kuwa uteuzi wa vijana wanaojiunga na mradi huu unafanywa na Viongozi
wa Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na vijana wanaoishi katika mazingira
magumu kwa kufata vigezo ambavyo ni; vijana wenye ulemavu, wasichana waliopata
watoto katika umri mdogo,vijana yatima au wanaolelewa na mzazi mmoja, vijana
wanaofanya kazi na kuishi katika mazingira hatarishi pamoja na vijana ambao
hawakumaliza shule kutokana na changamoto mbalimbali.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Leah
Lukindo ameushkuru Umoja wa Ulaya pamoja na waandaaji na watekelezaji wa mradi
huu wakiwemo Wizara ya Vijana na Ajira, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Stadi, Shirika la Plan International, Shirika la Volunteer Service Oversees
(VSO),CCBRT, UHIKI, CODERT pamoja na uongozi wa Serikali za Mitaa kwa
kuhakikisha mradi huu unaogusa hitaji kubwa la kitaifa la ajira kwa vijana unafanikiwa.
Wakiwasilisha
ujumbe kwa njia ya risala,vijana waliohitimu mafunzo hayo wamesema kuwa
wamepata msaada na ushauri ambao umewajengea ujasiri wa kuweza kujiajiri
wenyewe na hata kuajiriwa kutokana na fursa zilizopo na zitakazojitokeza.
Mradi
huu unatekelezwa katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi na
Mtwara kwa kipindi cha miaka mitatu, mradi huo unagharimu kiasi cha Euro
3,874,984.53 na unafadhiliwa na Umoja wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya.
No comments:
Post a Comment