‘Mbali
na utekelezaji wa agizo la Rais juu ya mkakati wa upatikanaji wa madawati,
suala hili linakwenda sambamba na ujenzi wa madarasa hivyo Serikali imeanza utekelezaji
wa ujenzi huo kwa maeneo machache hivyo ni
jukumu la halmashauri kuhakikisha mnaandaa mikakati ya kuongeza vyumba vya
madarasa’ alisema Majaliwa.
Aidha
Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa Serikali imeanza mkakati wa utekelezaji wa
mpango wa kutumia mfumo mpya wa
upandishaji madaraja walimu kwa kuwa mfumo wa uliuotumika awali haukuwa na tija kwa
maslahi ya walimu nchini.
Akipokea
madawati hayo Waziri mkuu alisema kuwa anajua shida iliyopo ya upungufu wa
madawati katika wilaya ya Temeke hivyo na kugawa madawati hayo katika shule
tatu zilizopo katika Wilaya hiyo ikiwemo shule ya msingi Chamazi, shule ya
msingi Mbande pamoja na shule ya msingi Majimatitu .
Kwa
upande wake Waziri wa Wizara Ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga alisema wizara yake ina jukumu la kuhakikisha
inaitangaza nchi ili kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi, na kuongeza
kuwa elimu bora ni msingi imara katika kufanikisha hilo.
Waziri
Mahiga alisema Ubalozi wa Kuwait nchini pamoja na Jumuiya ya Mabohora
wameikabidhi Serikali jumla 405 ili kuunga mkono jitihada za Rais ikiwemo.
“Serikali
ya Kuwait kupitia Ubalozi wake hapa nchini wametoa madawati 300 na kuahidi kutoa mengine 300 na Jumuiya
ya Mabohora nao wamechangia madawati 105” alisema Balozi Mahiga.
Kwa
mujibu wa Waziri Mahiga alisema watumishi wa Wizara yake walichanga kiasi cha
Tsh. Milioni 100 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha umma ili kuhamasisha umma
kuhusu zoezi la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na Sekondari
nchini.
No comments:
Post a Comment