![]() |
|
Wajumbe
waliohudhuria Ufunguzi wa Maadhimisho ya Sita wa Wiki ya Maji ya Afrika,
wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa,
leo Jijini Dar es Salaam
|
Na
Eleuteri Mangi
Viongozi
wanaoshiriki Ufunguzi wa Maadhimisho ya Sita wa Wiki ya Maji ya Afrika, na
Mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Maji barani Afrika (AMCOW) wameaswa kujadili
na kuona namna bora ya kuwapatia majisafi na salama wananchi waishio vijijini.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim
Majaliwa alipokuwa akifungua maadhimisho hayo yanayoshirikisha wadau wa maji barani Afrika na
ulimwenguni kwa ujumla leo jijini Dar es Salaam.
“Wananchi
waliopo vijijini bado wana uhitaji mkubwa wa maji, kwa kupitia mkutano huu
mawaziri wa maji, wataalamu wa sera na wadau wa maendeleo mkae pamoja, muone
namna sahihi ya kuwapatia watu maji” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa, kupitia mkutano huo wajumbe watajadiliana na kubadilishana
uzoefu ambapo Tanzania itanufaika kwa kuwa ina neema kubwa ya vyazo vingi vya
maji ikiwemo bahari, maziwa pamoja na mito, ambayo ni muhimu katika upatikanaji
wa maji kwa watanzania na nchi jirani.
Akitolea
mfano, Waziri Mkuu alisema kuwa kupitia Ziwa Victoria, Tanzania inapakana na
nchi za Uganda na Kenya, Ziwa Nyasa na Malawi pamoja na Msumbiji, na Ziwa
Tanganyika Tanzania inapakana na Zambia pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya
Kongo, ambapo vyanzo hivyo vya maji vinaweza kutumika kuwahudumia watu wa
maeneo hayo kwa manufaa ya maendeleo ya sekta mbalimbali.
Aidha,
Waziri Mkuu Majaliwa amesisitiza kuwa wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya
maji wavitunze ili wananchi wanaotegemea vyanzo hivyo waendelee kupata huduma
ya maji endelevu kwa matumizi mbalimbali.
Akizunguzia
namna Tanzania inavyoshiriki mkutano huo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa malengo ya Tanzania ni kuhakikisha kufikia
mwaka 2020, Serikali imedhamiria kufikisha maji katika maeneo yote nchini
ambapo kwa upande wa vijijini inatarajiwa kufikia asilimia 85 na asilimia 95
kwa upande wa mijini.
Waziri
Lwenge ameongeza Serikali imejipanga na kuipa Sekta ya Maji kipaumbele, ambapo
katika bajeti ya mwaka huu zimetengwa zaidi ya Sh. trilioni 1 na hadi kufikia
2030 Tanzania itakuwa imekamilisha miradi yote ya maji kwa asilimia 100. Hayo
yakiwa ni malengo ya nchi za Afrika ya kuwapatia wananchi wote mijini na
vijijini maji kwa asilimia 100 hadi kufikia mwaka 2030.
Akiwakaribisha
wageni waalikwa kwenye mkutano huo Rais wa AMCOW ambaye pia ni Waziri wa Maji
kutoka Senegal Amodou Mansour Faye alisema kuwa wajumbe wanawajibu wa kujadili
na kubadilishana uzoefu wakati wa mkutano na baada ya mkutano kwa manufaa ya
wananchi wa nchi wanazoziwakilisha.
Maadhimisho
ya Wiki ya Maji ya Afrika pamoja na Mkutano wa AMCOW unafanyika nchini kwa mara
ya kwanza yanaongozwa na kauli mbiu ya “Kufikia lengo la maendelevu (SDGs) juu
ya usalama wa maji na usafi wa Mazingira”.
Kwa
mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwake maadhimisho ya Wiki ya Maji ya Barani Afrika
na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Maji barani Afrika yalifanyika nchini
Tunisia mwaka 2008 katika mji wa Tunis, 2009 ulifanyika Mindrad Afrika ya
Kusini, mwaka 2010 Adids Ababa nchini Ethiopia, mwaka 2012 Cairo nchini Misri na mwaka 2014 mkutano huo ulifanyika 2014
Dakar Senegal.








No comments:
Post a Comment