Trending News

CCM Adverts and Promo

Sunday, July 10, 2016

WAZIRI MKUU WA INDIA AONDOKA NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, wakiwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumuaga Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akiagana na baadhi ya maafisa wa Serikali na raia wa India wanaoishi nchini, baada ya kuwasili  uwanja wa ndege wa Kiamataifa Julius Nyerere tayari kwa kuondoka nchini huku akisindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (aliyeinua mkono) akimueleza jambo mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati alipowasili uwanja wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa kuondoka nchini baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (aliyeinua mkono) akimueleza jambo mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati alipowasili uwanja wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa kuondoka nchini baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akimpungia mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na baadhi ya maafisa wa Serikali na raia wa India waliomsindikiza uwanja wa ndege wa Kiamataifa wa Julius Nyerere baada ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania.

Ndege ya India aliyopanda Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ikiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kukamilisha ziara ya siku mbili nchini Tanzania ambapo alisindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Askari wa Tanzania, akishusha Bendera ya Nchi ya India (kulia)  kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi kuondoka nchini baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya siku mbili aliyofanya nchini Tanzania.

Picha zote na Hussein Makame





No comments:

Post a Comment