Na
Pius Nkanabo, Dar es Salaam,
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole,
Augustino Lyatonga Mrema amewaonya polisi
jamii kuacha kujichukulia sheria mikononi kwa kuwapiga raia na kuwalazimisha wasichana
kufanya nao ngono kilazima.
Mazungumzo hayo
yamefanyika leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tandale, Mtaa wa
Pakacha ambapo Mwenyekiti wa Bodi hiyo ameahidi kutatua kero hiyo kwa
kuwachukulia hatua wananchi watakaojichukulia sheria mikononi.
“Polisi Jamii wamekuwa
ndiyo tatizo kubwa kwa wakazi wa eneo hili kwa kujichukulia mamlaka ya kuwatesa
na kuwanyanyasa wananchi hivyo, natoa tamko kwa yeyote atakae bainika kumkamata
mwananchi yeyote bila sababu ya msingi achukuliwe hatua za kisheria”, alisema
Mrema.
Mhe. Mrema ameongeza
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Poul Makonda ndiyo Mwenyekiti wa Usalama wa
Mkoa huu hivyo ni lazima amchongee kwa Rais kwa kuwa ameshindwa kuifanya vizuri
kazi yake ya kusimamia Jeshi la Polisi ipasavyo.
Aidha, Mwenyekiti wa
Bodi hiyo ameahidi kuwasaidia wanawake kwa kuwapa mikopo na kuwahakikishia
usalama wa biashara zao kwa kuwa waanawake wengi wamekuwa wakinyanyaswa na
kulazimishwa kufanywa ngono bila ridhaa yao.
Pia amewaonya wale wote
wanaowachukua wasichana kwa ajili ya kufanya kazi za nyumbani kutoka Mikoa
mbalimbali na kuwatelekeza au kuwapa kazi tofauti na walizowaitia watachukuliwa
hatua kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment