Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe ametangaza kuwa kwa sasa ni marufuku mtu kusafirisha kiholela wanyama hai kwenda nje ya nchi.
Prof Maghembe ameyasema hayo leo hii alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC1 ambapo pia ameahidi kuwatumia zaidi wanamichezo kama Mbwana Samatta katika kutangaza utalii.
#Prof Maghembe: Pamoja na kelele za Tanzania kuongeza kodi ya VAT katika utalii, takwimu zinaonesha watalii wameongezeka na mapato yameongezeka pia;
#Prof Maghembe: Hakuna mzungu anayetaka kuja kupumzika katika nchi yenye amani, utulivu na ukarimu kama Tanzania halafu akashindwa kuja kisa eti ada zimepanda kutoka USD 45 hadi USD 53 tu!;
#Prof Maghembe: Tanzania tuna vivutio vya utalii ambavyo havipo popote duniani kwa hiyo asikudanganye mtu kuingiza kodi ya VAT hakujawazuia watalii kuja;
#Prof Maghembe: Nilikuwa Berlin, Ujerumani hivi karibuni ukienda Balozi za Rwanda au Kenya ukikuta wametoa viza za watalii 10 kwa siku basi ukienda ubalozi wa Tanzania utakuta wametoa viza 100 kwa siku hiyo hiyo kwa watalii;
#Prof Maghembe:Mabalozi wetu nje ya nchi wanafanyakazi kubwa sana kuutangaza utalii;
#Prof Magjembe: Hivi sasa inajulikana wazi kuwa kweli unaweza kuuona Mlima Kilimanjaro ukiwa Kenya lakini pia watalii wanajua wazi kwamba utaupanda tu mlima huo iwapo uko Tanzania,
#Prof Maghembe: Utalii wa ndani bado una safari ndefu.Tukiutumia vyema tutaingiza fedha nyingi zaidi. Katika miaka mitano hii tutaongeza nguvu eneo hili;
#Prof Maghembe: Tunaalika wawekezaji waliojipanga katika ujenzi wa hoteli za kisasa za kitalii za nyota 7,6 au 5.Ukija kwangu umejipanga tunakupa eneo la kujenga ndani ya siku 7 tu;
#Prof Maghembe: Tumekomesha ujangiri kwa kutumia mbinu na teknolojia za kisasa za kuwasaka wahusika.Watumishi wa Tanapa na taasisi nyingine wanapewa mafunzo ya kijeshi kudhibiti ujangiri;
#Prof Maghembe: Hivi sasa ukikamatwa kwa ujangiri ni sawa na gaidi au mhujumu uchumi;
#Prof Maghembe: Tumewakamata watuhumiwa wakubwa wa ujangiri akiwemo anayeitwa "Malkia wa Pembe za Ndovu" na hakuna kigogo atakayesalimika bado tunawasaka wengine;
#Prof Maghembe pia ameulizwa na watazamaji kuhusu kumtumia mchezaji Mbwana Samatta kiutalii na ameahidi wataendelea kushirikiana na Wizara ya Michezo;
#Prof Maghembe: Marufuku kukata magogo au kuvuna maliasili ya misitu bila kibali.
#Prof Maghembe: Atakayekamatwa amevua magogo tutataifisha gari na mali iliyomo na mhusika atashtakiwa kama mhujumu uchumi.
#Prof Maghembe: watanzania tuna sifa nzuri ya ukarimu lakini tuwakatae wanaoendekeza wizi mdogo mdogo unatuchafulia sifa.
No comments:
Post a Comment