Mratibu wa
Huduma za Macho Mkoa wa Lindi Dk.Mwita Machage akimpima mgonjwa wa macho wakati
wa sikukuu ya Nane Nane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi leo.Huduma hii
ya upimaji wa macho imefadhiriwa kwa ushirikiano wa shirika lisilo la kiserikali la Sightsavers
Tanzania na sekretarieti ya mkoa wa Lindi Idara ya afya mkoa.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mheshimiwa George Simbachawene akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu shughuli
zinazofanywa na washirika wa utokomezaji wa ugonjwa wa vikope mkoani Lindi alipotembelea banda la Sightsavers na idara ya afya ya mkoa huo. Hadi wagonjwa 830 wamekwisha pata usawaziswaji wa vikope katika mkoa wa
Lindi, wilaya ya Ruangwa na Nachingwea. Kulia anayezungumza ni Dk. Leonard
Ndeki Afisa mradi kutoka shirika la Sightsavers Tanzania na Dk. Mwita Machage Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Lindi (katikati mwenye T-Sheti ya bluu).
Timu ya
washiriki toka shirika la Sightsavers na watumishi wa Idara ya Macho Mkoa wa
Lindi waliokaa wakiendelea kutoa huduma ya uchunguzi wa macho, Ushauri na Tiba kwa wananchi wa mkoa wa Lindi. Kutoka kushoto Dk. Mwita Machage, Dk. Leonard Ndeki
(Sightsavers), Bw. Richard Shaban na aliyesimama mwenye T-Shirt nyeusi ni Zera
Ombeni.
Baadhi ya wanawake na wanaume wa mkoa wa Lindi waliofika kwenye banda la Sightsavers na Idara ya afya mkoa kupata huduma ya macho
wakisubiria kupata huduma wakisubiri kuhudumiwa na wataalam wa Macho.
Spika Mstaafu wa Bunge
la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya Mhe. Anne Makinda akifurahia jambo na Wataalam wa huduma ya Macho kutoka Sekretariet ya Afya
Mkoa, Idara ya Macho na Sightsaver na wadau wa Mkoa wa Lindi walio katika kampeni ya kutokomeza
ugonjwa wa vikope chini ya ufadhiri wa mfuko wa Malkia Elizabeth wa
Uingereza.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Sightsavers Tanzania Bw. Gosbert
Katunzi (kushoto) akionyeshwa na Mratibu wa Huduma za
Macho Mkoa wa Lindi baadhi ya picha na maelezo mbalimbali ya wagonjwa waliokwishapata huduma ya
usawazishwaji na upasuaji wa mtoto wa jicho Mkoani Lindi kwenye banda la washirika
kati ya Sightsavers na idara ya afya mkoa wa Lindi wakati wa maonyesho ya Nane
Nane leo.
Mwananchi aliyefika katika banda la Huduma
ya Afya ya Macho akifanyiwa uchunguzi wa Macho katika maadhimisho ya sherehe za Nane
Nane mkoani Lindi leo.







No comments:
Post a Comment