Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wageni
mbalimbali waliohudhuria hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation
unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi,
usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani. Kwa mujibu
wa Hanns Seidel Foundation, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri
katika uwezeshaji wa wanawake.
Waziri wa Nchi, Kazi na
Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller akitoa uzoefu wa nchi ya Bavaria
katika kushughulikia masuala ya wanawake kupitia Sera zilizopo nchini humo wakati
wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha
na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na
masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula
(kushoto) ambaye ni miongoni mwa wanawake viongozi wa Tanzania walionufaika na
Mfuko wa Hanns Seidel Foundation akizungumza jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa hafla fupi ya
Tathmini ya Mafanikio ya Mfuko wa Hanns Seidel Foundation nchini Tanzania, jana
usiku jijini Dar es salaam.
Prof.Ursula Mannle, Mwenyekiti wa
Mfuko wa Hanns Seidel Foundation wenye makao yake nchini Ujerumani unaojihusisha
na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia
na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani akizungumza wakati wa hafla
fupi iliyoandaliwa na Mfuko huo jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Hanns
Seidel Foundation, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji
wa wanawake.
Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie
Müller (kulia) akifurahia picha ya kuchorwa aliyokabidhiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) jana jijini Dar
es salaam wakati wa hafla fupi
iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya
uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa
katika nchi mbalimbali duniani. Kushoto ni Prof.Ursula Mannle, Mwenyekiti wa
Mfuko wa Hanns Seidel Foundation wenye makao yake nchini Ujerumani.
Wageni mbalimbali
waliohudhuria hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha
na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia
na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani, jana jijini Dar es salaam.
Na.Aron Msigwa – Dar es salaam.
Mfuko wa Hanns Seidel Foundation (HSF) unaojihusisha na
uwezeshaji wa wanawake katika nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa
katika nchi mbalimbali umeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazofanya
vizuri katika uwezeshaji wa wanawake duniani.
Mwenyekiti wa Mfuko huo
ambao makao yake yako nchini Ujerumani Prof. Prof.Ursula Mannle ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati hafla fupi
iliyoandaliwa na mfuko huo kwa lengo la kufanya tathmini ya mchango wa HSF
nchini Tanzania katika kuwajengea uwezo wanawake vijana katika Nyanja za
uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa.
Prof. Ursula amesema kuwa HSF imekuwa ikitekeleza program mbalimbali za
uwezeshaji kwa wanawake kisiasa, kuwaandaa na kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi
mahiri katika nchi wanazotoka.
Amesema HSF imeamua kuanzisha programu maalumu nchini Tanzania kwa ajili
ya kuwaangalia wanawake wanaojitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali za
uongozi ili kuwawezesha kuwa viongozi katika nafasi mbalimbali serikalini pia
kuziba pengo lililopo la uwakilishi katika nafasi za kisiasa.
Ameeleza kuwa Hanns Seidel Foundation itaendelea kuwaunga mkono wanawake
wa Tanzania wanaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa nchini Tanzania
kupitia program mbalimbali za ufadhili ili kuwawezesha kumudu gharama na
kuwajengea uwezo wa kushindana katika majukwaa ya Siasa.
Waziri Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza
wakati wa hafla hiyo amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kutoa
kipaumbele katika nafasi za uongozi kwa wanawake.
Amesema licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake
vijana wa Kitanzania zikiwemo za kijamii na kimila pia ndoa na mimba za utotoni
zinazochangia vijana wanafunzi wa kike kuacha masomo yao, Serikali ya awamu ya
Tano imeamua kuja na Sera ya Elimu bure kuwawezesha vijana wa kike wa
kitanzania kupata elimu.
Amesema Tanzania imeendelea kuwathamini wanawake katika uteuzi wa ngazi
mbalimbali za uongozi Serikalini kuanzia wakuu wa Wilaya, Mikoa, Wakurugenzi,
Mawaziri na Naibu Mawaziri pia uwepo wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ni alama ya hamasa na ushindi katika
uongozi kwa wanawake wengine Tanzania.
Mhe. Mwalimu ameushukuru Mfuko huo kwa mchango wake katika kuwainua
wanawake wa Tanzania pia program mbalimbali zilizoanzishwa na mfuko huo kwa
lengo la kuwawezesha wanawake nchini.
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria
Emilie Müller akitoa uzoefu wa nchi ya Bavaria katika kushughulikia masuala ya
wanawake amesema kuwa kupitia Sera zinazosimamia masuala ya wanawake mambo
mengi yameweza kufanyika.
Ametoa wito kwa Tanzania kuendelea kuzishughulikia changamoto mbalimbali
ambazo zimekuwa kikwazo kwa wanawake wa Tanzania kufika mbali na kuwazuia
wasiweze kusimama wenyewe katika masuala ya Siasa.
Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa
jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula ambaye ni miongoni mwa wanawake wa
Tanzania walionufaika kutokana na HSF amesema kuwa alianza harakati za siasa
mwaka 2004 licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali.
Amesema kuwa ipo haja ya wagombea wanawake vijana wanaoingia katika
ulingo wa siasa kusaidiwa kifedha na mfuko huo pamoja na vyama vyao vya siasa
wanavyoviwakilisha pindi wanapogombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuongeza
kuwa wakati umefika kwa wanawake wanaoingia katika siasa kusimama wenyewe
kwenye majimbo ya uchaguzi.
Ametoa wito kwa HSF kuendelea kuwasaidia wanawake vijana wanaoingia kwa
mara ya kwanza katika masuala ya siasa kwenye chaguzi zinazokuja ili kuwawekea
mazingira mazuri ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili.






No comments:
Post a Comment