Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakabidhi zawadi baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao |
Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Mwenyekiti
wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Prof.Ninatubu Lema
|
Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi
ya mabanda wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kumi na Nne wa Bodi ya Wahandisi
nchini leo JIjini Dar es Salaam.
|
Baadhi
ya waandisi wakila kiapo cha kiapo cha utii katika kazi ya uhandisi mbele ya
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
|
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wahandisi kutoka nje ya nchi. |
Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha
ya pamoja na wakandarasi waliohudhuria mkutano huo.
Picha na Hassan Silayo
|
Na Sheila Simba-MAELEZO
Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka wahandisi nchini kufanya
kazi kwa weledi na uadilifu ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia ujezi
na uendelezaji viwanda.
Amesema hayo leo jijini Dar es salaam katika mkutano
wa 14 wa Bodi ya Wahandisi Nchini,na
kuwaasa kutumia taaluma yao kusaidia nchi kufikia uchumi wa kati ili kuleta maendeleo kwa haraka kwa watanzania.
“Mkiamua nchi iende kwenye uchumi wa kati
inawezekana lakini kama mtaamua isiendi pia inawezekana hivyo basi uzalendo
unahitajika katika kufanya kazi na kufikia malengo tuliyojiwekea,”Alisema Rais Magufuli.
Aidha amewataka kufanya kazi kwa
ushirikiano,kujitambua na kuaacha ubinafsi miongoni mwao hasa kwenye utendaji
kazi na miradi ya maendeleo.
“Tumemsikia Waziri akisema serikali inamapango wa
kukarabati na kununua meli mbili, wahandisi jiulizeni mmejipangaje kutumia
fursa hii kwa kuomba tenda na naamini serikali haiwezi kukataa ombi hasa kwa
wahandisi wa ndani”Alisema Rais Magufuli
Akimkaribisha rais Magufuli katika mkutano huo
waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa alisema kuwa licha
sekta ya miundo mbinu kufanya vizuri hasa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha
lami,Serikali itaendelea kulipa kipaumbele ujenzi wa barabara kuanzia viijiji,Halmashauri na za mikoa.
“Serikali inafanya jitahada kujenga miondo mbinu
imara ili kurahisisha usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda nyinfine na
ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma umekamilika kwa asilimia 98,” Alisema Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi
Prof.Ninatubu Lema amemuomba Rais kutoa nafasi kwa wahandisi wa ndani kushiriki
katika miradi mikubwa ili kujifunza kupitia miradi hiyo.
Aidha Mhandisi
Lema kwa niaba ya bodi hiyo wametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 100
kwaajili ya kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari
nchini.
akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Dar
Es Salaam Mhe.Paul Makonda alitangza tarehe mosi oktoba kuwa siku ya kupanda
miti katika mkoa wa Dae Es Salaam.
“Katika kuhakikisha miundo mbinu inakua safi natangaza
rasmi hapa tarehe mosi oktoba itakua ni siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dar
Es Salaamu na kampeni hiyi itaitwa MTI WANGU”alisema Makonda
No comments:
Post a Comment