Na
Ally Daud - Dar es salaam.
Hospitali
za Muhimbili, Amana, Mwananyamala na Kairuki za Jijini Dar es
Salaam zinatarajia kuwekwa kwenye mradi maalum wa kudhibiti taka hatarishi
ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuboresha usafi wa mazingira katika huduma za
afya nchini.
Mradi
huo wa kudhibiti taka hatarishi ikiwemo sindano,
gloves, nyembe na bandeji unasimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP)
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mazingira uliofanyika leo Jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Huduma ya aAfya na Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt.
Neema Rusibawengile alisema kuwa lengo la mradi huo una lengo la
kukabiliana na magonjwa ya maambukizi katika maeneo ya hospitali nchini.
“Mkutano
huu umelenga kuandaa na mradi utaodhibiti taka hatarishi amabao utanza
kufanya kazi katika hospitali za Muhimbili,Amana,Mwananyamala kairuki na
baadaye kuendelea nchi nzima” alisema Dkt Rusibawengile.
Dkt. Lusibamayila amesema kuwa mkutano huo pia
umewakutanisha wadau mbalimbali wa Maendeleo na Mazingira watakaojadili
mbinu mpya za kutunza mazingira kwa ajili ya kupeuka magonjwa ya
maambukizi nchini yanayotokana na taka hatarishi.
Kwa
mujibu wa Dkt Lusibamayila mkutano pia huo umelenga kupata njia
mbadala za kupunguza uzalishaji wa mekyuri katika hospitali, zahanati na vituo
vya afya ili kuondoa utumiaji wa vifaa vyenye nishati hiyo.
Kwa
upande wa mratibu wa udhibiti wa taka hatarishi za Hospitali Dkt. Honest
Anicetus amesema wadau wa mkutano huo pia wamepanga kubuni mikakati ya
kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya afya katika utunzaji wa
mazingira.
No comments:
Post a Comment