Hussein
Makame - Dar es salaam
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itazialika Asasi za Kiraia zinazotaka kutoa Elimu ya
Mpiga Kura kutuma maombi ya kupata kibali cha kutoa Elimu hiyo ili kuhakikisha kila
Mtanzania anapata Elimu ya Mpiga Kura.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.
Emmanuel Kawishe wakati akitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye kipindi cha Kumekucha
cha Televisheni ya ITV jijini Dar es Salaam leo.
Alisema
kwa kuanzia asasi hizo zitapewa muda wa miezi sita kupima mafanikio ya kutoa
Elimu hiyo na kwamba NEC itatoa kibali kwa asasi ambayo imetimiza vigezo vya
kutoa Elimu ya Mpiga Kura nchini.
Bw.
Kawishe alitaja vigezo hivyo kuwa ni asasi iwe imesajiliwa Tanzania, imefanya
kazi ya kutoa Elimu si chini ya miezi sita, iwasilishe majina ya viongozi wake,
iwe inaweza kujigharamia na iwasilishe anuani yake.
Aliongeza
vigezo vingine kuwa ni kama ni asasi ya
nje inayofanya kazi pamoja na Tanzania, kati ya viongozi wake wakuu watatu
wawili wawe ni Watanzania na isiwe na historia ya kuchochea machafuko ama ndani
ya Tanzania au nje ya Tanzania.
“Katika
kupata uhakika wa taarifa hizi, sisi Tume ya Taifa ya Uchaguzi hatuna taarifa
za kutosha kuhusiana na hizo asasi, kwa hiyo tunashirikiana na Jeshi la Polisi
na Msajili wa Asasi tutawaomba taarifa za asasi hizo ili kujiridhisha” alisema
Bw. Kawishe.
Alifafanua
kuwa NEC inahitaji kuzifahamu asasi zinazotoa Elimu ya Mpiga Kura ili kujihakikishia
zinatekeleze lengo ambalo tume hiyo inataka litekelezwe ambalo ni kutoa Elimu ya
Mpiga Kura kwa wananchi katika maeneo
wanayotaka kuitoa.
“Kwa
hiyo hizi asasi tutazialika, tutatoa tangazo kuanza na kumalizika kwa kipindi
na kuna watendaji ambao wameandaliwa rasmi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi
watakaokuwa wanaratibu asasi hizo, watakapoleta maombi yao watayapitia na kuona
je yanakidhi vigezo” alifafanua Bw. Kawishe.
Alisema
katika maombi yao asasi za kiraia zitaombwa kuainisha maeneo ambayo wanataka
kwenda kutoa Elimu hiyo lakini NEC itazisii kwenda kutoa Elimu hiyo maeneo ya
pembezoni ili kuifikisha Elimu ya Mpiga Kura katika maeneo hayo.
Bw.
Kawishe alisema NEC imeamua kutoa Elimu hiyo endelevu kwa kuwa tathmini
imeonesha kuwa Elimu hiyo haitolewi kama inavyotakiwa kiasi cha kuwafanya wananchi
wengi kutofahamu majukumu ya Tume na kutumia kadi ya kupigia kura kama
utambulisho kwenye taasisi za mikopo badala ya kupigia kura.
Mkurugenzi
huyo wa Huduma za Sheria wa NEC aliwataka Watanzania kuifuatilia Tume kwenye
mikutano ambayo itashiriki kutoa Elimu hiyo, kupitia kwenye vyombo vya Habari
au kuingia kwenye Tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kupata Elimu ya Mpiga
Kura.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi inatekeleza mkakati wa kutoa Elimu ya Mpga Kura nchini
ambapo imeshiriki kwenye Maonesho ya Sabasaba na Nanenane, ilishiriki Mkutano
wa Mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Wiki ya Vijana kitaifa
mkoani Simiyu na kutoa Elimu kwenye shule za Sekondari nchini.
No comments:
Post a Comment