#Tayari Serikali imeingia awamu ya pili ya utekelezaji wa programu ya maendeleo ya sekta ya maji nchini - Mhandisi Futakamba.
#Fedha kutoka katika Mfuko wa Maji kwa kiasi kikubwa zitaelekezwa kujenga miundombinu ya maji vijijini - Mhandisi Futakamba.
#Jumla ya wananchi 27,700,000 (72%) wanaoishi vijijini wanapata maji safi na salama- Mhandisi Futakamba.
#Wizara ya Maji na Umwagiliaji imeanzisha Jumuiya ya watumiaji maji katika maeneo yote yenye miradi hiyo ili kudhibiti uharibifu wa miundombinu ya maji - Mhandisi Futakamba.
#Hadi kufikia 2020 Serikali imejipanga kumaliza tatizo la maji kufikia 85% kwa vijijini na 95% kwa mijini - Mhandisi Futakamba.
#Serikali ina mipango ya muda mfupi ya kujenga visima sehemu zenye shida kubwa ya maji - Mhandisi Futakamba.
#Miradi ya majisafi ambayo imeshakamilika ni; Dodoma mjini na UDOM, Nansio, Sengerema, Ruvu chini na Ruvu juu- Mhandisi Futakamba.
#Mradi wa maji wa Dodoma mjini na UDOM unazalisha maji lita milioni 61.5 - Mhandisi Futakamba.
#Miradi ya maji ikikamilika itasaidia katika kuimarisha uchumi wa viwanda nchini -
Mhandisi Futakamba.
#Wizara inategema kuanzisha miradi miwili ya uondoaji wa majitaka Jijini Dar es Salaam - Mhandisi Futakamba.
#Jumla ya hekta 461,000 ziko chini ya miradi ya kilimo cha umwagiliaji- Mhandisi Futakamba.
#Hekari 461,000 zinazotumia kilimo cha umwagiliaji zinachangia 24% ya chakula kinachozalishwa nchini - Mhandisi Futakamba.
Imeandaliwa na Idara ya Habari (MAELEZO)
No comments:
Post a Comment