Trending News

CCM Adverts and Promo

Monday, June 23, 2014

MAADHIMISHO YA WIKI YA WAZAZI TANZANIA.


Umoja wa Wazazi Tanzania kila mwaka huadhimisha wiki ya Wazazi ambayo huadhimishwa kuanzia tarehe 1-6 April kila Mwaka.
Kitaifa Mwaka 2014 maadhimisho hayo yaliadhimishwa Kisiwani Pemba, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Alhaj Abdalah Majura Bulembo (MCC). Na kila Mkoa waliadhimisha wiki hiyo katika mikoa yao Kwa kufanya shughuli mbalimbali za Kijamii ikiwemo Usafi wa Mazingira, upandaji miti na kutembelea watoto yatima na waathirika wa HIV na madawa ya kulevya.
Mkoa wa Morogoro waliadhimisha wiki ya Wazazi katika Wilaya ya Mvomero  ambapo Makatibu na Wenyeviti wa Wilaya zote za Mkoa huo walihudhuria.






Katika maadhimisho hayo Mkoa wa Morogoro uliadhimisha kwa upandaji miti katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko Wilayani humo ambapo Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa Ndugu Shaweji.



No comments:

Post a Comment