Trending News

CCM Adverts and Promo

Tuesday, February 16, 2016

Mhe.Ummy Mwalimu Ashusha Rungu Kwa Wakurugenzi wa MSD

TUMBUA Majipu’ ya Serikali ya awamu ya tano, kwa mara nyingine tena imewafika vigogo wanne wa Taasisi ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kutokana na tuhuma za kuwepo matumizi mabaya ya Sh bilioni 1.5.hatua iliyoisababishia Serikali hasara.
Uamuzi wa kuwasimamisha kazi vigogo hao ambao ni Mkurugenzi wa Kanda wa MSD, Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Fedha, Joseph Tesha, Mkurugenzi wa Ugavi, Misanga Muja na Mkurugenzi wa Manunuzi, Heri Mchunga umefikiwa jana na WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Mhe.Ummy Mwalimu

Mh Mwalimu ametoa agizo la kusimamishwa wakurugenzi hayo kwaMwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD
“Naomba uwaandikie barua za kuwasimamisha wakurugenzi hawa wanne ili wapishe uchunguzi wa matumizi mabaya ya Sh bilioni 1.5 za MSD,” alisema Ummy alipozungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam.
Ummy alisema taarifa alizonazo ni kwamba kiasi hicho cha fedha, kilitumika kununulia dawa kinyume cha utaratibu na Sheria ya Manunuzi ya Umma, hivyo kuna haja ya kufanyika kwa uchunguzi huo.
Uamuzi wa Waziri huyo wa Afya ni mwendelezo wa hatua kadhaa zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano dhidi ya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ubadhirifu kwa kuchukuliwa hatua katika kile ambacho Rais John Magufuli amekipachika jina la ‘kutumbua majipu.’

No comments:

Post a Comment