Trending News

CCM Adverts and Promo

Thursday, March 24, 2016

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MIUNDOMBINU YA TAIFA YA KUSAFISHIA GESI KUTOKA MTWARA

 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakikagua Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba mkoani Mtwara, 
 Baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakijadiliana jambo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini katika Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba mkoani Mtwara hivi karibuni. Kutoka kushoto ni Afisa wa Bunge Amon Marco, Mhandisi Godson Chacha, Afisa wa Bunge Msaidizi (Madini) Andendekisye Mbije, Afisa wa Bunge Msaidizi (Nishati) Kalory Mmasy na Mhandisi Robert Dulle.
 Meneja Mkuu Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba (wa pili kushoto), akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, walipokuwa katika ziara kukagua Mradi huo mkoani Mtwara hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msimbati, alipokuwa katika ziara pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kukagua Mradi wa Bomba la Gesi. 

No comments:

Post a Comment