Na
Jacquiline Mrisho -Dar es Salaam
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe amepokea taarifa ya utafiti wa
marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka Tume ya kurekebisha Sheria.
Akipokea
taarifa hiyo leo Jijini Dar es salaam Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe amesema
taarifa hiyo ya utafiti itasaidia kurekebisha sheria ya manunuzi ambayo inalenga
kukuza uchumi wa nchi.
“Mimi
na wataalamu wangu tumeipokea taarifa hii, tutaiangalia na kuhakikisha
tunaifikisha Wizara ya Fedha na Mipango na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili
kuendelea na utaratibu unaofuata ili mchakato wa marekebisho uweze kufanyika
kwa haraka”alisema Dkt Mwakyembe.
Akifafanua
juu ya sheria ya manunuzi ya Umma, Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji
Aloysius Mujulizi amesema kuwa Tume
imefanya utafiti wa sheria hiyo kwa kushirikisha wadau mbalimbali.
“Tumepata
maoni mengi na ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi na wasimamizi wa manunuzi
ya Serikali kwa namna wanavyoiona sheria ya manunuzi ya Umma,na sisi tumeyachambua
maoni hayo kwa kutumia vigezo vya sheria”alisema Jaji Mujulizi.
Aidha,Tume
imetoa maoni kwa Serikali kusimamia sheria ili iweze kuendana na ukuaji wa
uchumi nchini kwa kurekebisha baadhi ya sheria ili kuepuka muingiliano uliopo
kati ya sheria ya manunuzi na sheria nyingine.
Marekebisho
ya sheria hii ni moja ya agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.
John Pombe Magufuli lililotolewa Novemba
2015 alipokua akizindua Bunge la 11.
No comments:
Post a Comment