Trending News

CCM Adverts and Promo

Thursday, March 17, 2016

MWIGULU AONYA KUHUSU MAUAJI YA KISIASA

WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi,  Bw. Mwigulu Nchemba amesema hakuna chama cha siasa ambacho kinaweza kuthaminishwa na maisha ya mwanadamu na kwamba wananchi hawana sababu ya kupigana na kutoanabugai kwa sababu ya ushabiki wa vyama.

Ametoa kauli hiyo  wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Katoro, wilayani Geita alipopewa nafasi kuwasalimia wananchi kwenye mkutano wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. 

"Duniani kote hakuna chama cha siasa kinaweza kuwa na thamani sawa na maisha ya mwanadamu au damu ya mwanadamu. Ninazungumza hili nikihusisha na matukio ya hivi karibuni hapa Geita na kule Tunduma ambako raia wetu walipoteza maisha kwa sababu ya tofauti za kisiasa, "alisema.

Aliwauliza wananchi hao ni kwa nini wanapigana hadi kutoana uhai wakati wao (wananchi) hawaendi bungeni. "Ninyi mnaopigana hakuna hata mmoja wenu anayeingia bungeni lakini sisi tukikutana kule bungeni tunasalimiana na kugongeshana glasi. 

Akitolea mfano kauli hiyo, Waziri Mwigulu alisema wakati wanakwenda kwenye msiba wa wana CCM waliouawa huko Tunduma, baada ya mazishi yeye na Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe pamoja na wanasiasa wengine walikaa pamoja na kula nyama za kuchoma hadi usiku.

"Nini kinachowafanya muwe maadui wa siasa kiasi hicho?" alihoji na kuongeza : "Mnasababisha watoto wasio na hatia tena wasiojua siasa wawe yatima. Duniani siasa hazina tofauti kama zilivyo mechi za mpira. Leo unavaa jezi hii na kesho jezi ile. Acheni kufanya uadui katika siasa", alionyam Mhe. Mwigulu.



No comments:

Post a Comment