Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume ya Taifa Bw. Kailima Ramadhani
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema haitambui kujitoa kwa Chama cha Wananchi (CUF), katika uchaguzi wa Mbunge Jimbo la Kijitoupele hapa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Jumapili licha ya kuwa Tume imepokea barua rasmi toka kwa uongozi wa Chama hicho.
Mkurugenzi
wa uchaguzi wa Tume ya Taifa Bw. Kailima Ramadhani amesema Tume imefikia maamuzi
hayo kutokana na ukweli kuwa barua hiyo ya CUF imechelewa huku maandalizi ya uchaguzi huo yakiwa
yamekamilika na ni Wananchi tu kwa sasa Wanasubiriwa kwenda kupiga kura.
Aidha,
Bw. Kailima ameeleza kuwa, kwakuwa karatasi za kupigia kura zilishachapishwa na
kuwasili hapa nchini tayari kwa uchaguzi huo, zitaendelea kuwa na picha za Wagombea
wa CUF hata kama wamejitoa katika uchaguzi huo.
Awali,wajumbe
wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji mstaafu
Hamid Mahamood Hamid walitembelea katika vituo mbalimbali vya kupigia kura katika
Jimbo la Kijitoupele ili kujiridhisha na maandalizi ya uchaguzi huo kabla ya uchaguzi
kufanyika jumapili.
Tume
ilibaini kuwepo kwa baadhi ya kasoro ndogo ndogo katika baadhi ya vituo vya kupigia
kura ikiwa ni pamoja na kubanduliwa kwa karatasi zenye majina ya wapiga kura, mfano
katika kituo cha Skuli ya sekondari Kinuni.
Jimbo
la Kijitoupele lina jumla ya Wapiga kura wapatao 17,274 na vituo vipatavyo 53
vitatumiwa na wapiga kura ili kumchagua mbunge waJimbo la Kijitoupele siku ya Jumapili.
Sambamba
na Uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Kijitoupele, marudio ya uchaguzi mkuu wa
Zanzibar Oktoba 25,2015 ambayo matokeo yake yalifutwa uatafanyika Jumapili hiyo
pia.
Uchaguzi
katika jimbo la Kijitoupele uliahirishwa mwaka jana kutokana na hitilafu ndogo ndogo
zilizojitokeza katika karatasi za kupigia kura, kabla ya kufutwa kwa matokeo ya
Uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, 2015.
No comments:
Post a Comment