Halmashauri mpya ya Wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro imeanza rasmi zoezi la kuhakiki watumishi hewa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wapya wa mikoa wakati akiwaapisha Machi 15 mwaka huu,Ikulu jijini Dar es salaam.
Mhe.Rais aliwaagiza Wakuu wa Mikoa kutoa maelekezo kwa Wakurugenzi na Wakuu wa wilaya kuhakikisha kuwa wanasimamia zoezi la kuhakiki na kuwaondoa watumishi hewa katika orodha ya malipo ya mishahara ya mwezi Machi, 2016 ndani ya siku 15.

Zoezi hilo katika Halmashauri mpya ya wilaya ya Malinyi linaendeshwa na watumishi wa Idara mbalimbali ikiwemo Idara ya Utumishi, Afya, Elimu, Maafisa Tarafa pamoja na Wakuu wa Idara na vitengo kutoka katika wilaya hiyo.

No comments:
Post a Comment