Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia)
akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair
alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair
alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini
Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za
Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia
Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia)
akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe.
Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo
Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja
na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika
nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia
alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi
Arabia.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na
wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia uwekwaji saini wa mkataba kuhusu
Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara,
Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa
na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia
iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na
wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia kubadilishana hati baada ya
uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia
katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa
upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na
Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al
Jubair.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi
Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Picha/IKULU.





No comments:
Post a Comment