Trending News

CCM Adverts and Promo

Friday, April 8, 2016

HAPA KAZI TU: CCM YAJIBU MAPIGO YA LOWASA


 Msemaji wa Chama. Cha Mapinduzi Ndugu Christopher Ole Sendeka akiongea na waandishi wa Habari.


Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa,Ap
rili 7, 2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu
vya ndani na nje ya nchi.

Katika mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa
yakiwemo hali ya siasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma
mbalimbali, na kile alichokiita tatizo la mfumo nchini.

Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala
yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais
John Pombe Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake
wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla.

Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani mifumo
iliyopo, iliyowekwa tangu awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na
imekuwa ikiboreshwa kulingana na mahitaji.

Ifahamike hakuna mahali popote duniani ambako mfumo wa nchi unajiendesha
wenyewe, siku zote mfumo huongozwa na kuendeshwa na binadamu ambao kwa
udhaifu wa ama kibinadamu au wa kukusudia, hufanya makosa yanayohitaji
kusahihishwa kwa taratibu zilizowekwa.

Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali
ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa
ili  kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na
matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.

Chama Cha Mapinduzi kina ushahidi wa utendaji wa Ndugu Lowasa akiwa Waziri
Mkuu namna alivyoendesha zoezi la kusimamisha na kufukuza kazi na
kuwadhalilisha watumishi bila kufuata taratibu, hali hiyo ni tafauti sana
na hii ya sasa, kwani kila anayesimamishwa kazi, anasimamishwa kwa kufuata
taratibu zote, ili kuhakikisha kila mtumishi anatendewa haki ya kusikilizwa.

Na katika hili la kuwasimamisha kazi watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa
ufisadi, wizi na matumizi mabaya ya ofisi, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea
kuunga mkono, kutokana na baadhi yao kuwa chanzo cha  shughuli za maendeleo
nchini.

Kiongozi au mwanasiasa anayemkosoa Rais Magufuli katika hatua anazozichukua
hivi sasa, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma,
ni kutiliwa shaka kwani kufanya hivyo ni sawa na kutetea wizi, ufisadi na
uporaji wa rasilimali za nchi.

Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM

No comments:

Post a Comment