Trending News

CCM Adverts and Promo

Tuesday, April 12, 2016

HABARI KATIKA PICHA ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA MKOANI MOROGORO:

OUSAFI WA MAZINGIRA: Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Bulembo  akifyeka majani katika eneo la Hospitali ya Mkoa wa Morogoro wakati wa maadhimisho ya Miaka 61 ya Umoja wa Wazazi yaliyfanyika kitaifa mkoani Morogoro. Katikati ni Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Morogoro Bi. Mecktridis Mdaku
UZINDUZI WA MASHINA: Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Morogoro Ndugu Seif Shaban Mohamed akifungua mashina katika wilaya ya Morogoro mjini maeneo ya Sultan Area.

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Morogoro Ndugu Seif Shaban Mohamed akifungua mashina katika wilaya ya Morogoro mjini maeneo ya Sultan Area.
 UTOAJI WA TUZO MBALIMBALI: Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Morogoro Bi. Mecktridis Mdaku akisoma Tuzo za marafiki wa wazazi ambao walikabidhiwa tuzo hizo na Mwenyekiti wa Wzazi Taifa wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya Umoja wa Wazazi Tanzania
Usafi wa mazingira ukiendelea katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro
Vijana wa Chipukizi wakiwa katika Gwaride maalum la mapokezi ya Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Bulembo wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya Umoja wa Wazazi Tanzania yaliyofanyika  mkoani Morogoro.
Vijana wa Chipukizi wakimvika Skafu Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Bulembo wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya Umoja wa Wazazi Tanzania yaliyofanyika  mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Bulembo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wazazi na CCM mkoa wa Morogoro wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya Umoja wa Wazazi Tanzania yaliyofanyika  mkoani Morogoro.
 Moja ya Shina la Umoja wa Wazazi -CCM lililofunguliwa wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhiwa CD yenye nyimbo za umoja wa Wazazi.

UPANDAJI WA MITI:  Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Morogoro Bi. Mecktridis Mdaku akipanda mti ikiwa ni sehemu ya utunzaji wa mazingira wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya Umoja wa Wazazi Tanzania
 Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Morogoro Bi. Mecktridis Mdaku akizungumza katika moja ya kikao cha Wazazi mkoani humo wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya Umoja wa Wazazi Tanzania
Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Bulembo (kushoto) akizungumza na mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Lyamuya mara baada ya kufanya usafi katika hospitali hiyo
UTOAJI WA MISAADA: Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndugu  Bulembo (kushoto) akikabidhi
 msaada wa vitu kwa makundi mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho hayo.


Na.Mwandisi Wetu- Morogoro.

 Umoja wa Wazazi Tanzania, Jumuiya ya CCM Morogoro umeadhimisha miaka 61 ya wazazi Tanzania kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira katika hospitali ya mkoa wa Morogoro  na baadaye  kukabidhi vyandarua 100 ,shuka 100 pamoja na vifaa vya usafi. Msaada huo umegharimu shilingi milioni 2.5.

Pia wametembelea kituo cha watoto wenye mtindio wa ubongo cha Amani Centre na kutoa msaada wa vyakula mbalimbali vilivyogharimu shilingi milioni  1.2.



Aidha,Umoja huo umetoa vitendea kazi zikiwemo kompyuta pamoja na mashine za kuduufu zenye thamani ya shilingi milioni 12  kwa Wilaya Saba Mkoa wa Morogoro ambazo ni Ulanga, Morogoro mjini, Morogoro Vijijini, kilosa, Gairo, Mvomero, na Kilombero. Vitendea kazi hivyo vimegharimu.

Ukiacha vitendndea  kazi hivyo pia wamekabidhi  vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 4.8. Vitabu hivyo ni vya masomo ya Sayansi (Fizikia, Baiolojia, na Kemia, pia vitabu vya Hisabati, Jiografia, Kiingereza, Historia pamoja na TEHAMA. Vitabu hivyo walipatiwa shule ya mkono wa Mara ya kilosa na Wilaya ya Malinyi.












No comments:

Post a Comment