Trending News

CCM Adverts and Promo

Friday, April 15, 2016

RAIS WA SUDAN YA KUSINI, MHE. JENERALI SALVA KIIR MAYARDIT AWASILI NCHINI KWA AJILI YA ZIARA YA KIKAZI.


Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) ambayo ilimbeba Rais wa Sudani ya Kusini, Mhe. Jeneral Salva Kiir Mayardit ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (mwenye tai nyekundu) akielekea kumpokea Rais wa Sudani ya Kusini, Mhe. Jeneral Salva Kiir Mayardit baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akishuka katika ndege ya Shirika la Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (wa tatu kushoto) akiwa tayari kumpokea Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (kushoto) akisalimiana na Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja jijini Dar es Salaam.


Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (wa tatu kulia) akisalimiana na Kamanda Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Siro  mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuja kumpokea mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akipita katikati ya gwaride la Jeshi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja.

Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga wakielekea kupanda magari tayari kwa safari ya kuelekea Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gari lililombeba Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit likiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere Jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Benedict Liwenga- MAELEZO)

No comments:

Post a Comment