Na
Jacquiline Mrisho
Mamlaka
ya Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa makampuni binafsi ya ulinzi yanayofanya
kazi bandarini hayahusiki na ulinzi wa sehemu nyeti za za Mamlaka hiyo.
Akitoa
ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi.
Janeth Ruzangi amekiri kuwepo kwa makampuni yanayofanya kazi ya ulinzi
bandarini na amefafanua kuwa hayahusiki kwa namna yoyote ile kulinda sehemu za
ndani za ofisi zilizoko bandarini.
“Ninapenda
kuwafahamisha wananchi kuwa Bandari inalindwa na walinzi wa aina tatu ; Jeshi
la polisi, Polisi wasaidizi walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania
(Auxilliary Police) pamoja na walinzi wa Makampuni binafsi”
Ameongeza
kuwa makampuni hayo yanalinda maeneo ya nje ya bandari yakiwemo maegesho ya
magari ya watumishi wa mamlaka kama ilivyo kwenye ofisi nyingine.
Aidha,amefafanua
kuwa Polisi wa bandari walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania wako kwa
mujibu wa sheria zilizotungwa na Bunge na wamepata baadhi ya mafunzo ya
kipolisi.
Ikumbukwe
kuwa agizo la kuwandoa walinzi wa makampuni binafsi kwenye maeneo nyeti ya
bandari lilitolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mwezi Februari mwaka huu
alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo.

No comments:
Post a Comment