|
Wanachama wa Jumuiya
ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiimba wimbo
wa Taifa wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Jumuiya hiyo ulifanyika jijini
Dar es Salaam.
|
(Na Lorietha Laurence- Dar es salaam).
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe.George Simbachawene
ameifuta Bodi ya usimamizi wa jengo la Machinga Complex la jijini Dar es salaam
na kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda kulisimamia kwa kuhakikisha kuwa linatumiwa na wafanyabiashara wadogo wasiokuwa na maeneo
maalum ya kufanyia biashara.
Ametoa agizo hilo
Leo jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa jiji hilo wakati wa
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya
wafanyabishara Tanzania(JWT).
“Naomba Mkuu wa mkoa usimamie jengo hili kwa
kuhakikisha wale wafanyabiashara wadogowadogo waliopo pembezoni mwa barabara
maeneo ya karume na wengine wasio na sehemu za kufanyia kazi kufanya biashara
zao hapo” alisema Mhe Simbachawene
Amesema
wafanyabishara hao wanatakiwa kunufaika kwa kupatiwa maeneo maalum ya kufanyia
kazi huku akieleza kuwa ni wajibu wa serikali kuhakikisha inatenga maeneo hayo
ikiwemo machinga complex ambayo ipo kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo.
Amewataka Wakuu wa
Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuwa walezi wa Jumuiya za Wafanyabiashara katika mikoa
na wilaya zao ili kupata nafasi ya kukaa pamoja na kujadili matatizo mbalimbali yanayowakabili na
namna ya kuyatatua.
Pia ameziagiza
Halmashauri kutokutumia nguvu katika kukusanya kodi bali washirikiane na
wafanyabiashara ikiwemo kuwapatia elimu ya
umuhimuwa ulipaji kodi ili kuwepo na uwazi na uwajibikaji kati ya pande zote mbili.
“Naomba tuondokane na
dhana ya mgambo kunyang’anya wafanyabiashara bidhaa zao na badala yake uwekwe
utaratibu wa kuwapatia elimu ya mlipa kodi
ili waweze kutambua umuhimu wa kulipa kodi kwa hiyari kwa maendeleo ya Taifa ”
alisema Mhe.Simbachawene.
Waziri
Mhe.Simbachawene pia ameahidi kusimamia uwazi na uajibikaji katika ulipaji kodi
kwa kuhakikisha kuwa sheria na taratibu
za ulipaji kodi zinafuatwa na kuzingatiwa na hivyo kuondokana na kodi elekezi
ambazo zinapelekea mianya ya rushwa kwa
watendaji wa serikali na wafanyabiashara na hivyo kuliletea taifa hasara.
Aidha amesema kuwa
atayasimamia mapendekezo yaliyotolewa na Jumuiya hiyo ya Wafanyabiashara ikiwemo
uwazi na uwajibikaji katika ulipaji wa kodi bandarini ,utoaji wa lesini uwe kwa
kipindi cha miaka mitano au mitatu na udhibiti wa utoaji holela wa lesini za
biashara kwa wafanyabiashara wageni.
Kwa Upande wa
Mwenyekiti wa Jumuiya Ya Wafanyabiashara Tanzania Bw.Johnson Minja ametoa wito
kwa serikali kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ili kuwa na walipa kodi
halali watakaokuza uchumi wa nchi kutoka uchumi wa kati hadi uchumi wa viwanda
na hivyo kukuza pato la taifa.
No comments:
Post a Comment