Trending News

CCM Adverts and Promo

Wednesday, May 4, 2016

CCM YASHINDA KESI YA UBUNGE JIMBO LA MAFINGA



Mbunge wa jimbo la Mafinga Bw Cosato Chumi akiweka sawa bendera ya Mbunge kwenye gari lake kabla ya kuondoka viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa baada ya kushinda kesi ya uchaguzi dhidi ya mgombea wa CHADEMA ,kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Ndugu Jimson Mhagama.

  ******************************************************"*****************
CHAMA CHA MAPINDUZI  wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimempongeza mbunge wa jimbo la Mafinga Mhe. Cosato Chumi baada ya kushinda kesi yake ya uchaguzi dhidi ya aliyekuwa mgombea ubunge jimbo hilo kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Bw Willy Mungai .

Akizungumza na wanahabari leo nje ya viwanja wa mahakama kuu kanda ya Iringa baada ya mahakama kutoa huhukumu iliyompa ushindi Mhe. Chumi ,katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Ndugu  Jimson Mhagama alisema kuwa baada ya hukumu hiyo ya mahakma kumpa haki mbunge huyo wa CCM kazi kubwa iliyobaki kwa sasa ni kuona utekelezaji wa ilani ya CCM unafanywa kwa nguvu zote.

“Hapa kwa hukumu hii haki imeweza kutendeka kwani kabla ya kutoa hukumu jaji alisoma na kutolea ufafanuzi wa vipengele vyote ambavyo mlalamikaji alikuwa anavilalamikia na baada ya hapo ndipo alipoweza kutoa hukumu ya kesi hiyo “

Hata hivyo amesema pamoja na hukumu hiyo kutolewa bado wanachama wa Chadema na wale wa CCM katika jimbo la Mafinga hawana budi kuendelea kuwa wamoja ili kushikamana na mbunge wao kuleta maendeleo jimboni .

No comments:

Post a Comment