Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba amelieleza Bunge mjini Dodoma akifafanua kuwa kwa kipindi kirefu mazao ya wakulima yamekuwa yakitozwa ushuru yanapofika mipaka ya kata kwenye mageti maalumu na hata yanaporudishwa mashambani, hali ambayo imekuwa ikilalamikiwa sana na wakulima nchini.
Akiwasirisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni Dodoma Katika mwaka ujao wa fedha amesema wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa Sh 275,063,518,000.
. Mhe. Mwigulu ametangaza neema kwa wakulima kwa kuwaambia kuwa pembejeo za kilimo sasa zitapatikana kwa wingi.
. Mhe. Mwigulu ametangaza neema kwa wakulima kwa kuwaambia kuwa pembejeo za kilimo sasa zitapatikana kwa wingi.
Amesem wizara inapitia upya mfumo wa sasa wa vocha za pembejeo kwa lengo la kupata mfumo utakaowezesha upatikanaji wa mbolaea kwa wakulima wote wanaohitaji kupitia maduka ya pembejeo kwa bei nafuu.

No comments:
Post a Comment