Habour Master Kapteni Abdul Mwengamuno kutoka Mamalaka ya
Bandari ya Dar es Salaam(kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt
Leonard Chamriho (kushoto) hatua za kuzingatia wakati wa upakuaji wa mafuta
kutoka kwenye meli mpaka kwenye mita za kupima mafuta ambapo mafuta hayo
huchujwa kuondoa uchafu kwa kupitia mitambo maalum iliyofungwa kwenye mita
hiyo.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akipanda ngazi
kuelekea kwenye pampu na valvu zilizofungwa kwenye mita ya kupimia mafuta(Flow
Meter) wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua utendaji kazi wa mita
hiyo.
Mita
ya Kupimia Mafuta (Flow Meter) iliyojengwa eneo la kwa mwingira, mji Mwema
Kigamboni jijini Dar es salaam .
Utaratibu wa kujenga uzio na paa kufunika mtambo huo unaendelea kupitia
mkandarasi aliyepewa jukumu la kujenga mradi huo ili kukuimarisha ulinzi na
usalama wa mita hiyo. Picha/Raymond Mushumbusi na Aron Msigwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi Dkt. Leornad Chamuriho ameupa siku mbili uongozi wa Bandari unaosimamia Mita ya Kupimia mafuta nchini (Flow Meter) iliyoko Kigamboni jijini Dar es salaam kuhakikisha kuwa unatoa taarifa ndani ya siku mbili kuhusu hitilafu iliyojitokeza kwenye mfumo wa umeme wa kufungua valvu za mita hiyo.
Aidha, ameuagiza uongozi huo kutoa taarifa kuhusu hitilafu ya kamera 2 za usalama zilizoungua na kushindwa kufanya kazi kwa takribani mwezi mzima.
Katibu Mkuu huyo ametoa maagizo hayo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika mita hiyo eneo la mji Mwema Kigamboni jijini Dar es salaam leo ambapo alibaini mapungufu katika utendaji wa baadhi ya maeneo.
Ameyataja hayo kuwa ni pamoja na kamera za kufuatilia mwenendo wa usalama wa mita hiyo, valvu zilizoshindwa kufanya kazi upande wa mfumo wa umeme hivyo kubakiwa na njia ya analoji kutokana na hali ya mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha jijini Dar es salaam.
“Ifikapo Jumatatu
nipatiwe taarifa kuhusu matengenezo ya vifaa hivi, hatua zilizochukuliwa na
mnieleze lini ukarabati wake utakamilika pia ujenzi wa paa kuzuia athari ya mvua kwenye mita hii” amesema Dkt. Chamuriho.
Ameongeza kuwa
dhumuni la Serikali ni kuhakikisha vifaa hivyo vinafanya kazi katika viwango vinavyostahili ili kulinda
mapato yanayotokana na mafuta yanayoingia nchini ili Serikali ipate kodi halali
na hivyo kuongeza mapato ya nchi na kuondoa malalamiko kwa wateja.
Kwa upande wake Meneja Mradi wa Ujenzi wa Mita hiyo kutoka Mamlaka ya
Bandari nchini Mhandisi Mary Mhayaya ameeleza kuwa uharibifu wa vifaa
hivyo umesababishwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na tayari vifaa hivyo vimeanza kukabarati.
" Kisichofanya kazi ni mfumo wa kufungua mafuta upande wa umeme kwenye baadhi ya valve, upande wa analoji unafanya kazi vizuri na kazi ya upakuaji mafuta kupitia mfumo wa analojia inaendelea kama kawaida" Amesisitiza.
Amesema kuwa tayari wamemweleza mkandarasi aliyefunga vifaa hivyo kuvifanyia marekebisho haraka iwezekanavyo.
Naye Kaimu
Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Hebel Mhanga amesema kuwa ofisi yake
inajukumu la kuhakikisha inatoa huduma sahihi kwa wateja wanaotumia mitambo
hiyo iliyopo bandarini hapo na Serikali
inapata mapato kulingana na huduma iliyotolewa.
Mita ya
Kupimia Mafuta yalnayoingia nchini iko katika
hatua ya majaribio kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo tayari meli tatu zimefanyiwa
majaribio ya upakuaji wa mafuta huku moja ikiwa imefanyiwa vipimo.
No comments:
Post a Comment