Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) Dkt. Jabiri Bakari akizungumza na Wahariri wa vyombo vya Habari jijini Dar es salaam
Na. Aron
Msigwa – Dar es salaam.
SERIKALI
kupitia wakala ya Serikali mtandao imesema kuwa inaendelea kulifanyia kazi suala
la uanzishaji wa mfumo wa TEHAMA utakaowawezesha wananchi kupata huduma na
taarifa mbalimbali za Serikali kupitia simu zao mkononi mahali popote walipo
kwa njia ya mtandao.
Utaratibu huo
pia utawawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali vya elimu nchini Tanzania kupata
taarifa za ajira za Serikali na kuwawezesha kuomba nafasi hizo, kufuatilia
majibu ya usaili walioufanya na kupata
taarifa za kuitwa kazini kupitia namba za utambulisho watakazopewa kupitia
ujumbe mfupi (sms).
Akizungumza na
Wahariri wa vyombo vya Habari jijini Dar es salaam Mtendaji Mkuu wa Wakala
ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) Dkt. Jabiri Bakari amesema kuwa mfumo huo utamuwezesha mwananchi kupata huduma
za Serikali mahali popote alipo kufuatia mifumo ya TEHAMA kuwasiliana na
kubadilishana taarifa.
Amesema kuwa
dhana ya Serikali Mtandao ni kuwa na matumizi
ya TEHAMA kwenye shughuli zote za Serikali kwa lengo la kuongeza ufanisi na
kupunguza gharama za uendeshaji kwenye huduma za Afya, Utalii, Malipo ya tozo
za huduma,vibali, leseni ,elimu na huduma mbalimbali za Serikali.
Dkt. Jabiri
amesema moja ya vitu vinavyosababisha
usumbufu kwa wananchi kutokana na kukosekana kwa Serikali mtandao ni pale
wanapohitaji kupata huduma za Serikali ikiwemo Hati ya kusafiria ambapo hulazimika
kwenda Idara ya Uhamiaji kujaza fomu maalum na kisha kusubiri kwa muda wa zaidi
ya wiki moja ili taarifa zao ziweze kuhakikiwa na taasisi nyingine za Serikali
wakati suala hilo lingeweza kuchukua siku moja.
“Matumizi ya
TEHAMA kwenye shughuli za Serikali hurahisiaha sana upatikanaji wa taarifa kwa kuwa mifumo inawasiliana na kubadilishana
taarifa haimlazimu mwananchi kwenda kwenye taasisi zaidi ya tano kupata huduma
yake” Amesisitiza Dkt. Jabiri.
Amesema taasisi
za Serikali kama Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara
ya Uhamiaji, RITA na taasisi nyingine ambazo majukumu yao hutegemeana kupitia
serikali mtandaomifumo ya taasisi hizo huunganishwa ili ifanye kazi pamoja kwa
lengo la kuruhusu mifumo kuzungumza kumuhudumia
mwanachi bila yeye kulazimia kuzifuata taasisi hizo.
Amesema kuwa
pamoja na maboresho mbalimbali yanayoendelea ndani ya Serikali ya kujenga Serikali mtandao imara mfumo uliopo
sasa kwenye baadhi ya taasisi humfanya mwananchi achukue muda mrefu kupata
huduma.
Ameeleza kuwa
taasisi za Serikali zinazofanya kazi katika mazingira yanayofanana
zinaposhirikiana katika kutoa huduma Kupitia Serikali mtandao mwananchi wa
kawaida hatajua nini kinaendelea, atakachokipata mwisho ni majibu ya huduma aliyoiomba
kama ni Bandarini atachukua mzigo bila
usumbufu wowote kwa kuwa suala la kodi, upakuaji na upakiaji wa mizigo na
ukaguzi halitamgusa mwananchi.
Ameongeza kuwa
ili Serikali mtandao iweze kufanya kazi yake ipasavyo nchini lazima kuwe na
miundombinu ndani ya taasisi au nje pia uwepo wa mifumo Tumizi ( Application
Systems) inayoshughulikia masuala mbalimbali, wafanyakazi pamoja na Sera,
miongozo na taratibu za kusimamia TEHAMA
kuwezesha huduma mtandao ( e - Servieces).
Dkt. Jabiri
amesisitiza Tanzania iko kwenye hatua ya kwanza na ya pili, kwa maana ya
taasisi nyingi za Serikali zina tovuti zenye taarifa za awali za kumsaidia mtu
kujua nini kinapatikana au kutolewa na taasisi za serikali ili aweze kuchukua
hatua ya kupata huduma.
Amesema Wakala
ya Serikali mtandao imefanikiwa kuweka mifumo kwa maana ya Tovuti kuu ya
Serikali, Tovuti ya Wananchi, Tovuti ya data huria ambayo ina taarifa
mbalimbali za wananchi kuhusu Maji, Barua pepe ya Serikali (GMS) ambayo sasa
inatumiwa na jumla ya taasisi 117 za Serikali na Balozi mbalimbali kwa lengo kuepuka
matumizi ya barua pepe za muda.
Amebainisha
kuwa Wakala ya Serikali Mtandao kwa sasa eGA katika awamu ya kwanza imeziuganisha
taasisi 75 za serikali na Wizara zote za Serikali kupitia mkongo wa taifa, pia
Wakala imeziunganisha Taasisi 72 zilizounganishwa kwa simu zinazotumia itifaki ya
Intaneti kwenye mkongo wa taifa ili kurahisisha mawasiliano na kupunguza
gharama.
Akijibu Suala
la baadhi ya Taasisi za serikali kukawia kuunganishwa kwenye mtandao amesema
kuwa awali hakukuwa na mfumo huo kutokana na baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza
kwenye Sera, miongozo na taratibu zinazosimamia utendaji wa shughuli za kila
siku serikali lakini sasa kuna mwongozo wa taasisi kuzingatia ili kuhakikisha
mifumo ya taasisi za Serikali inawasiliana ili kufanya kazi pamoja kuondoa
mapungufu yaliyokuwepo.
Aidha, mifumo
ya utendaji kazi inabadilika kulingana na mabadiliko yanayotokea kwenye taasisi
hizo na kuongeza kuwa Wakala ya Serikali mtandao imekuwa makini sana
kuhakikisha hakuna mfumo unaoinuka dhidi ya mwingine lengo likiwa kumhakikishia
mwananchi kupata huduma katika eneo moja kwa muda mfupi.
Kwa upande
wake Meneja Habari,Elimu na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan Mshakangoto
amesema kuwa suala la matumizi ya mitandao mbalimbali isiyo rasmi katika
shughuli za serikali linafanyiwa kazi huku akisisitiza kwamba utaratibu
unaandali wa kuhakikisha kuwa mawasiliano yote ya matumizi ya barua pepe nje ya
zile za serikali kwenye ofisi za umma yanafungwa kuanzia Saa 1:30 hadi saa 9:30.
Kwa sasa ni
taasisi 72 tu za serikali zikiwemo Wizara zote, Wakala, Bunge na taasisi
zimeunganishw, Aidha halmashauri 77 zimeunganishwa na mkongo wa taifa na kazi
ya kuzifikia taasisi zote 500 inaendelea ili kuwezesha zoezi la kufunga huduma
za mawasiliano za serikali nje ya mkongo wa taifa.
Takribani
taasisi 200 za umma zina tovuti ili kurahisisha upatikanaji wataarifa na huduma
kwa wananchi. Changamoto iliyopo ni Tovuti nyingi kukosa taarifa zilizohuishwa
pia kuunganisha maeneo ambayo bado hayajafikiwa hasa Halmashsuri na vijiji ili
kuwezesha taarifa mbalimbali kupatikana kwa wakati.
Wakala imepata
mafanikio katika utekelezaji wa jitihada za Serikali mtandao hasa katika
uwekaji wa mifumo ya Serikali kwa maana ya Tovuti kuu ya Serikali, Tovuti ya
Wananchi, Tovuti ya data huria ambayo ina taarifa mbalimbali za wananchi kuhusu
Maji, Barua pepe za Serikali ambayo sasa ina taasisi 117 na Balozi mbalimbali
zinatumia GMS ili kuepuka matumizi ya barua pepe za muda.
Wakala ya
Serikali Mtandao katika awamu ya kwanza imeunganisha taasisi 72 za serikali na
Wizara zote za Serikali kupitia mkongo wa taifa pia imeziunganisha taasisi hizo
na simu zinazotumia itifaki ya intaneti kwenye mkongo wa taifa ili kurahisisha
mawasiliano na kupunguza gharama.
Akifafanua
kuhusu hatua ya mifumo ya serikali kuchelewa kufanya kazi pamoja amesema hapo
awali hakukuwa na mfumo uliowezesha jambo hilo kufanyika kutokana na baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye
Sera, miongozo na taratibu zinazosimamia masuala ya TEHAMA nchini lakini sasa
kuna mwongozo uliotolewa kuhakikisha mifumo ya taasisi za Serikali
inawasiliana na kufanya kazi pamoja ili kuondoa mapungufu yaliyokuwepo.
Aidha, mifumo
ya utendaji kazi inabadilika kulingana na mabadiliko yanayotokea kwenye taasisi
hizo na kuongeza kuwa Wakala ya Serikali mtandao imekuwa makini sana
kuhakikisha hakuna mfumo unaoinuka dhidi ya mwingine lengo likiwa kumhakikishia
mwananchi kupata huduma katika eneo moja kwa muda mfupi.
Meneja Habari,
Mawasiliano Suzan Mshekangoto amesema suala la matumizi ya mitandao mbalimbali
isiyo rasmi katika shughuli za serikali linafanyiwa kazi huku akisisitiza
kwamba utaratibu unaandaliwa kuhakikisha kuwa mawasiliano yote ya matumizi ya
barua pepe nje ya zile za serikali kwenye ofisi za umma yanafungwa kuanzia Saa
1:30 hadi saa 9:30 alasiri.
Amefafanua
kuwa taasisi 72 za serikali zikiwemo Wizara zote, Wakala, Bunge na Mahakama zimeunganishwa,
Aidha halmashauri 77 zimeunganishwa na mkongo wa taifa na kazi ya kuzifikia zilizobaki
inaendelea ili kuwezesha mawasiliano ya serikali kupita kwenye mkongo wa taifa.
Bi. Suzan amesema
mpaka sasa takribani taasisi 200 za umma zina tovuti zenye taarifa za huduma
mbalimbali zinazotolewa na Serikali huku Changamoto iliyopo ni baadhi ya Tovuti hizo kukosa
taarifa zilizohuishwa.
No comments:
Post a Comment