Trending News

CCM Adverts and Promo

Wednesday, May 11, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI NCHINI UGANDA KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS MUSEVENI UGANDA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na vikundi vya burudani vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana  na wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Uganda mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride rasmi la vikosi vya ulinzi vya Uganda aliloandaliwa  mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (Kushoto) na Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakipigiwa nyimbo za Taifa za Tanzania na Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.Picha/IKULU

No comments:

Post a Comment