Trending News

CCM Adverts and Promo

Wednesday, May 11, 2016

Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” wawasili mkoani Tanga.


Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha Dkt. Mohammed Alawi akiongea na baadhi ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani, ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.

Mtaalamu wa Maabara Apolinary Mushi anayefanya kazi katika zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Katy Migiro wa Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara mkoani Arusha kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.

Baadhi ya dawa zilizoidhinishwa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutibu ugonjwa wa malaria nchini.

Moja ya mabango yanayosambazwa nchini kuhamasisha wananchi kufanya vipimo dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Tanga.

Eneo la ukingo wa Bahari ya Hindi mkoani Tanga ambapo karibu na eneo walipofikia waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara yao mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.(Picha/Eleuteri Mangi, Tanga)

No comments:

Post a Comment