Na.
Beatrice Lyimo-MAELEZO,Dar
es salaam.
Serikali
imeipatia Mamkala ya Vitambulisho vya Taifa NIDA shilingi bilioni 2.3 (Bilioni
mbili na milioni mia tatu) kwa ajili ya kuwalipa watumishi wa muda 597 wa
mamlaka hiyo waliosimamishwa kazi hivi karibuni.
Taarifa
iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es salaam imesema kuwa
malipo hayo yanahusisha mishahara yao ya miezi minne na mshahara wa mwezi mmoja
wa notisi ya kusimamishwa kazi pamoja na malimbikizo ya madeni yao katika
mifuko ya hifadhi ya jamii.
Taarifa
hiyo imefafanua kuwa kabla ya kuwalipa watumishi hao Wizara ya Fedha ilifanya uhakiki wa mahojiano
ya ana kwa ana na watumishi hao pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali zikiwemo
majalada, mikataba ya ajira na madaftari ya mahudhurio, taarifa za kazi za kila
siku pamoja na namba zao za akaunti ya benki zilizokuwa zikitumika kulipia
mishaara ili kujidhihirisha kama madai hayo yalikuwa sahihi.
Mbali na hayo taarifa hiyo imeeleza kuwa katika uhakiki huo wizara ilibaini kulikuwa na kasoro kadhaa za kimikataba kati ya NIDA na watumishi hao.
Aidha,imeeleza kuwa wakati wa zoezi hilo jumla ya watumishi 597 walipaswa kuhakikiwa na kuongeza kuwa majina 565 ndio yaliyowasilishwa kuhakikiwa ambapo watumishi 516 walijitokeza katika zoezi hilo na watumishi 49 hawakujitokeza.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo
Watumishi
472 kutoka Tanzania bara na Tanzania visiwani ndio waliokidhi vigezo vya
kulipwa stahili zao za kuachishwa kazi huku 121 wakibainika kuwa na kasoro
mbalimbali ambazo zinapaswa kurekebishwa na Menejimenti ya NIDA kabla ya malipo
hayo.
Ikizitaja
baadhi ya kasoro hizo zilizobainika katika ukahiki huo ni pamoja na kusekana
kwa mikataba na majalada yao katika Ofisi ya mwajiri, kukosekana kwa majina yao
kwenye daftari la mahudhurio kazini, kuwa na utata kwenye mikataba, kufanana
kwa namba za majalada na kukosekana kwa barua za kusitishwa kazi.
Kufuatia
uhakiki huo, Wizara ya Fedha na Mipango imemaliza kazi yake ya Uhakiki na
kwamba jukumu la kuwalipa watumishi wa NIDA wanaostahili limeachwa mikononi mwa
Menejimenti ya NIDA.
No comments:
Post a Comment