***********************************************************************************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema viongozi wakuu wa nchini na washiriki wa mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa wamevutiwa na jitihada ambazo Tanzania imezichukua kukabiliana na janga hilo.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema viongozi wakuu wa nchini na washiriki wa mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa wamevutiwa na jitihada ambazo Tanzania imezichukua kukabiliana na janga hilo.
Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa,
Mei 13, 2016) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wake kwenye mkutano wa siku
moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani
uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.
Waziri Mkuu alisema katika
kikao cha kwanza kilichohudhuriwa na wakuu wa nchi na viongozi wa kitaifa
wapatao 20, alipata fursa ya kuelezea jinsi Tanzania ilivyoweza kupambana na
rushwa kwa kuzingatia vigezo vikuu vinne.
Waziri Mkuu alivitaja
vigezo hivyo kuwa ni kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazohusu masuala
ya rushwa; uanzishwaji wa mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza
kazi Julai, mwaka huu; mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya wananchi na
utaratibu wa kubaini wala rushwa kwa kushirikisha jamii ikiwemo kutunza siri za
watoa taarifa.
“Ziko sheria ambazo
zinafanyiwa kazi hivi sasa ambazo ni lazima zipitishwe na Baraza la Mawaziri
kabla mahakama hii haijaanzishwa, zikishapitishwa na Baraza ndipo zitaanza
kutumika,” alisema.
Akifafanua kuhusu mikakati
ya udhibiti wa fedha za miradi ya maendeleo, Waziri Mkuu alisema kwamba katika
bajeti ya mwaka huu, Serikali imeweza kuongeza kiasi cha fedha zilizotengwa kwa
shughuli za maendeleo kutoka asilimia 27 hadi kufikia asilimia 40.
“Kuongezeka kwa kiwango
hiki ni ishara tosha kuwa tumelenga
kutoa huduma kwa Watanzania na muhimu katika rushwa ni udhibiti wa fedha hizo
na kuhakikisha zinakwenda kwenye miradi; matuizi mazuri ya fedha za Serikali,
matumizi mazuri ya fedha zinazochangiwa na wahisani ili ziweze kutekeleza miradi
iliyokusudiwa,” alisema.
“Tumekubaliana na uwepo wa
uwazi na kushirikishana taarifa hasa katika kupeana taarifa za makampuni yanayoanzishwa
na kusajiliwa katika nchi zinazoendelea kama njia ya kudhibiti tabia ya nchi
ndogo kama Ireland na Panama kupokea na kuficha fedha zinazotoka kwenye nchi
zinazoendelea” alisema.
Alisema kila nchi
imesisitizwa kutumia raia na kuwalinda watoa siri, kutumia mifumo ya
kiintelijensia, kutumia wanasheria na kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya watu
wanaokamatwa kwa masuala ya rushwa.
Waziri Mkuu alisema alipata
fursa ya kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. David Cameron ambaye mbali
na kupongeza juhudi za Serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika
kupambana na rushwa pia aliahidi kutoa mwaliko ili Tanzania iweze kushiriki
kwenye mkutano mwingine wa masuala ya rushwa utakaofanyika Japan, Julai mwaka
huu.
“Anataka Tanzania iende
kwenye mkutano huo ili ikaelezee mafanikio iliyoyapata katika kukabili suala
hili, ili pia nchi nyingine ziweze kuiga utaratibu ambao Serikali imeutumia
hadi tukafanikiwa katika mapambano dhidi ya rushwa,” alisema Waziri Mkuu.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ofisi yake haijahusika na kuandaa mkutano
wa wanadiaspora waishio Uingereza kama ambavyo imedaiwa na baadhi ya watu kwenye
mitandao ya kijamii kwamba kuna watu maalum wamechaguliwa kushiriki mkutano huo.
Amesema mkutano huo
umepangwa kufanyika kesho (Jumamosi, Mei 14, 2016) na uko wazi kwa Watanzania
wote kushiriki ili waje kusikiliza nchi yao imefanya nini na kama kuna masuala
yanahitaji ufafanuzi, watapatiwa fursa hiyo.
“Kulikuwa na hofu ya watu
wanaotoka mbali kutoweza kushiriki sababu ya gharama, lakini nasema yeyote mwenye
uwezo wa kuja aje ndiyo maana tumeuweka muda wa asubuhi ili watu waweze
kushiriki na kuwahi kurudi makwao,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU.
No comments:
Post a Comment